Thursday, October 27, 2016

MCHUNGAJI RWAKATARE KUWATOA WAFUNGWA WENGIINE 43 GEREZANI KWA KUWALIPIA FAINI ZAO

Chief Hope | 2:22:00 PM | Toa maoni yako hapa!
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Assemblies of God (Mlima wa Moto), Getrude Rwakatare amesema ataendelea na mpango wake wa kuwanusuru wafungwa wanaotumikia adhabu magerezani kwa kuwalipia faini ili warejee uraiani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, alisema katika awamu ya pili ameamua kuwalipia wafungwa 43 waliopo katika magereza ya Mkoa wa Dodoma.

"Kampeni hii ya kuwalipia faini kati ya Sh 50,000 hadi 200,000 wafungwa waliopo magerezani imetupa moyo na Watanzania wengi wameguswa na hata kutupongeza. Kutokana na hali hii kanisa letu sasa limefanya hivyo tena na safari hii tunaelekea mkoani Dodoma," alisema.

Mchungaji Rwakatare alisema kesho watawatoa wafungwa hao mkoani Dodoma ambapo vigezo walivyoangalia ni wanawake wanaonyonyesha, wagonjwa na wazee.

"Nasi tunatimiza maandiko ya Mungu katika kufanya hivi na kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Parole, Augustino Mrema," alisema Mchungaji Rwakatare.

Alisema kutokana na makosa mbalimbali ya faini waliohukumiwa nayo wafungwa hayo, kanisa lao limetoa Sh milioni 6.8 kwa ajili ya kulipia faini hizo.

Awali Rwakatare kupitia kanisa lake, aliwalipia wafungwa 78 katika magereza matatu ya Keko, Segerea na Ukonga ya jijini Dar  es Salaam na kuachiwa huru baada ya kulipa faini ya Sh milioni 25 zilizochangwa na waumini wa kanisa hilo.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA 7 MWAKA 2016 HAPA.

Chief Hope | 1:25:00 PM | Toa maoni yako hapa!
Serikali imetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la 7 kwa mwaka 2016 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.52 na shule iliyoongoza kitaifa ni shule ya Msingi Kwema ya mkoani Shinyanga.

Bofya hapa kutazama

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

MAGONJWA 10 HATARI YANAYOTIBIKA KWA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA.

Chief Hope | 11:42:00 AM | Toa maoni yako hapa!
Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna kama mimi. Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo:

1. Ugonjwa wa moyo
2. Huimarisha kinga ya mwili
3. Huongeza uwezo wa macho kuona
4. Kinga ya kisukari
5. Dawa bora ya usingizi


Soma: Unazifahamu Faida Za Kula Tunda La Tikiti Maji? Ziko Hapa.


6. Dawa bora ya uvimbe
7. Huongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha
8. Dawa nzuri kwa matatizo ya tezi dume
9. Zinaongeza nguvu za kiume

10. Zinaondoa pia msongo wa mawazo (stress)

Namna nzuri ya kula mbegu za maboga:
Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 15 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.

Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

KAZI NZITO ZACHANGIA KUHARIBIKA UJAUZITO.

Chief Hope | 11:04:00 AM | Toa maoni yako hapa!
Inaweza kuonekana kama utani lakini utafiti uliofanyika hivi karibuni nchini Marekani unaonyesha kuwa wanawake wanaofanya kazi kwa zaidi ya saa 40 kwa wiki wapo kwenye hatari ya kushindwa kushika ujauzito.

Utafiti huo uliofanyika katika chuo kikuu cha Havard umeenda mbali zaidi na kueleza kuwa wanawake wanaobeba mizigo mizito pia wapo kwenye hatari hiyo.

"Matokeo yameonyesha kuwa ubebaji wa vitu vizito na ufanyaji kazi kwa muda mrefu, humsababisha mwanamke kuchelewa kupata ujauzito au kushindwa kabisa kushika mimba," alisema Audrey Gaskins ambaye ni kiongozi wa wataalamu walioshiriki kwenye utafiti huo.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

MAMBO 7 YANAYOPELEKEA WATU WENGI KUYAOGOPA MAHUSIANO.

Chief Hope | 10:56:00 AM | Toa maoni yako hapa!
1. Hofu ya kupoteza uasili wake binafsi. 
2. Hofu ya kukataliwa. 
3. Uzoefu duni wa zamani. 
Inajulikana kuwa hivyo ulivyo leo (utu na tabia) ni matokeo ya matukio mbalimbali uliyoyapitia tangu ukiwa mtoto. Ndio maana linapotokea jambo ambalo linahitaji maamuzi yako unalihukumu kwa kuhusianisha na uzoefu wa mambo uliyopitia hapo zamani 
4. Hofu ya kutodumu kwa mahusiano hayo. 

Soma: Mambo '5' Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuanza Uchumba.

5. Uhusiano mpya huathiri wa zamani. 
6. Upendo huwa hauwasili peke yake.
Upendo unapoingia maishani mwako huwa hauji peke yake, huja na majukumu, muda mwingi na haja ya nafasi kwa wapendwa wako. 
7. Matarajio yasiyo ya kweli.


By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

MUSIC VIDEO: KIU YANGU - ANGEL BENARD.

Chief Hope | 8:42:00 AM | Toa maoni yako hapa!
Nimekusogezea video mpya kutoka kwa mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili Angel Benard, video ya wimbo huu inaitwa KIU YANGU ikiwa imetengenezwa ndani ya studio ya DOXA Music.
By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

RAIS MAGUFULI AMETAJWA KUWANIA TUZO YA 'FORBES AFRICA PERSON OF THE YEAR.'

Chief Hope | 8:15:00 AM | Toa maoni yako hapa!
Rais Dkt John Pombe Magufuli ametajwa kuwania tuzo ya 'Forbes Africa Person of The Year.'

Anachuana na watu wengine wanne wakiwemo: Rais wa Mauritania, Ameenah Gulib, Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel Le Roux na Thuli Madonsela wa Afrika Kusini pamoja na watu wa Rwanda.


Zimebaki siku 22 za kupiga kura. Unaweza kumpigia kura Rais Magufuli kwa kubonyeza hapa. Hadi sasa Rais Magufuli anaongoza kwa asilimia nyingi (73%).


Mwaka huu tuzo hizo zitatolewa jijini Nairobi, Kenya November 17.


Wafuatao ni washindi wa tuzo hiyo miaka ya nyuma


Mohammed Dewji (Tanzania)– 2015

Aliko Dangote (Nigeria)– 2014
Akinwumi Adesina (Nigeria) – 2013
James Mwangi (Kenya) – 2012
Sanusi Lamido Sanusi (Nigeria)- 2011

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

TAZAMA MAGAZETI YA LEO OCTOBER 27, 2016.

Chief Hope | 7:23:00 AM | Toa maoni yako hapa!
Soma headlines za magazeti ya leo kuanzia kwenye, habari za kitaifa na michezo, ili ujue kinachoendelea.
By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

Wednesday, October 26, 2016

JE WE NI MPENZI WA INSTAGRAM?

Anitha Dallo | 1:48:00 PM | Toa maoni yako hapa!

Kama wewe ni mpenzi wa instagram hii ni habari njema kwako, Sasa instagram inpatikana kwenye computer yako kama unatumia window 10 na tablet.

TAMBUA KAULI YA RAIS MSTAAFU WA TANZANIA MH JAKAYA KIKWETE ILIYOLETA MIJADALA KWENYE MITANDAO YA JAMII

Anitha Dallo | 1:34:00 PM | Toa maoni yako hapa!

Katika sherehe za miaka 55 ya chuo kikuu ya dar es salaam mh. Jakaya kikwete akisoma hotuba yake alisema maneno yafuatayo

 ''unapokua mpya lazima watu waone kuna  mambo mapya lakini mapya ya maendeleo na sio mapya yanayobomoa kule tulipotoka''

HUYU NDIO MTU MWENYE UZITO MKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI

Anitha Dallo | 12:53:00 PM | Toa maoni yako hapa!
Iman Ahmad Abdulati kutoka Egypt ni mwanamke mwenye kilo 1102 na anamiaka 36 tangu akiwa na miaka 25 hajawahi kuamka kitandani.

ILI UFANIKIWE, USIOMBE RUHUSA BALI UOMBE MSAMAHA .

Richard Edward | 12:07:00 PM | | Toa maoni yako hapa!
 ILI UFANIKIWE, USIOMBE RUHUSA BALI UOMBE MSAMAHA .
Katika hali ya kawaida watu wengi hususani jamii yetu ya Kitanzania vijana wengi wanashindwa kuchukua hatua mapema katika maisha yao kwa sababu tu ya mfumo tuliouzoea na kisingizio kikubwa bado wanajipanga na kujipanga siku zote hakutimii ni bora uingie katika mapambano kuliko kujifunza nje ya mapambano. 

Karibu tujifunze "kwa nini usiombe ruhusa na uombe msamaha".

Na zifuatazo ni sababu 11 kwa nini usiombe ruhusa na uombe msamaha; 

1. Ili Usikatishwe Tamaa; 

Katika hali ya kawaida ukijaribu kufanya jambo ambalo linaweza kukuletea mafanikio na ukiomba ruhusa lazima utakatishwa tamaa, utaambiwa vikwazo vingi badala ya kupewa msaada katika jambo hilo. 

Isikupite Hii: Yusufu Na Rungu La Yesu - Tunza Imani Na Usikate Tamaa!

Lakini kama umejiunga na kundi la waasi wa mema ndio njia pekee ya kufikia kile tunachotaka katika maisha yetu. 

2. Ujifunze ; 

Siku zote mtu anayejaribu anajifunza sana kuliko yule mtu ambaye hajaribu. sasa ukiwa mtu wa kuomba ruhusa kwa kila kitu utajifunzaje? Ndio maana unashauriwa kuomba samahani kuliko ruhusa ili uweze kujifunza uingie kwenye mapambano ya dunia. 

3. Uweke Historia; 

Ukitaka mafanikio hapa duniani basi thubutu kufanya bila ya kupewa ruhusa kwa wazazi, walezi au ndugu. Ukifanya jambo zuri nao wakilikubali baadae watakuheshimu sana na utakuwa umejenga historia kubwa. 

Maisha ni muda na maisha ni marefu kama ukitumia vizuri muda wako. Sasa kama maisha ni muda kama mpaka sasa bado hujaanza mchakato au harakati za kujikomboa unasubiri nini? tumia vema rasilimali ya ujana ambayo ni nguvu na muda utaokoa maisha yako ya uzeeni. 

4. Uweke Heshima; 

Utapata heshima kutoka kwa jamii, ndugu, wazazi, jamaa na marafiki kama ukifanya jambo ambalo litagusa maisha ya watu wengine. 

Isikupite Hii: Mambo Sita (6) Yatakayo Weza Kukutopotezea Heshima Yako

Ili upate heshima amka sasa na nenda kapambane wewe tayari ni mshindi bado kukabidhiwa kombe tu na huwezi kukabidhiwa kombe ukiwa umelala inabidi uamke na uende kwenye mapambano. 

5. Ujenge Nidhamu Binafsi; 

Nidhamu ndio kila kitu katika maisha yako ili uweze kufikia mafanikio yoyote yale hapa duniani. Kama umepanga kuamka saa 11 ujisomee uongeze maarifa ulishe ubongo wako chakula cha asubuhi, huwezi kuamka kama huna nidhamu. 

Kwa hiyo nidhamu ndio kila kitu lenga kuwa na nidhamu itakukomboa katika kila idara hapa duniani na kumbuka nidhamu haiji kwa kuomba ruhusa jiongoze na jisimamie mwenyewe utapata matokeo chanya na siyo hasi. 

6. Ukumbane na Changamoto; 

Hakuna maisha bila changamoto, kila mtu hapa duniani ana changamoto zake, kwa hiyo changamoto zitakufanya ukue na ukomae kama huna changamoto basi wewe hujaribu kufanya mambo makubwa unafanya kile ambacho kila mtu anafanya. 

Isikupite Hii: Hatua Tano Za Uhakika Za Kutatua Tatizo Lolote Unalokutana Nalo

Na wakati mwingine changamoto zinaweza kukufanya kuwa mjasiriamali bora kwa sababu utaziona fursa, kama hujaribu basi huwezi kuziona fursa kwa jicho la tatu jaribu leo na usikate tamaa 

7. Utajijengea Uhusiano Mzuri na Jamii; 

kama unaweza kufanya mambo mema basi jamii iliyokuzunguka itakuwa imenufaika katika kile unachofanya jamii itaonja mchango wako na hivyo utakuwa umejijengea uhusiano mzuri na jamii

Ili ufanikiwe unatakiwa ujenge uhusiano mzuri na jamii na huwezi kufanikiwa bila watu. 

8. Utajijengea Falsafa ya Maisha Yako; 

Watu wengi wanaishi lakini wanaishi katika falsafa za maisha ambazo siyo zao. Kwa hiyo ni vizuri kujijengea falsafa ya maisha yako mwenyewe hapo utaishi maisha ya furaha

Usikubali kuishi maisha ya furaha ya kununua ishi maisha ya furaha ya asili. Mfano wa furaha ya kununua ambayo ni ya muda mfupi ni kama vile kuvuta sigara, kutumia vilevi ili upate furaha tu ya muda mfupi tafuta furaha ya kudumu na ya asili acha kuwa mtumwa wa kutafuta furaha ya kununua kila siku. 

9. Utajijengea Uwezo wa Kufikiri; 

Kuna tofauti kati ya kufikiri na kuwa na mawazo, kufikiri ( ni kutafuta jawabu chanya katika maisha yako na kuchukua hatua.) 

Mfano hali uliyo nayo sasa huridhishwi nayo kwa hiyo utachukua hatua chanya ya kukabili tatizo. Kama wewe ni binadamu na uko hai basi usiache kufikiri na kujifunza kwani kile ambacho hukijui huwa kinakufanya uwe masikini. 

10. Utajijengea Juhudi na Maarifa; 

Ukifanya kazi kwa juhudi na maarifa utajijengea ufanisi na utakuwa shujaa na shujaa ni alama ya ushindi

Jaribu kuthubutu kila siku  usisubiri mpaka uombe ruhusa wewe fanya uje uombe msamaha baadaye. 

11. Utaziona Fursa; 

Bilionea Richard Branson anasema fursa ziko kama magari barabarani moja linakwenda na lingine linarudi

Kama wewe umekaa tu huwezi kuziona fursa na bahati hutokea pale fursa inapokutana na maandalizi

Acha kulalamika chukua hatua utaziona fursa nyingi sana katika jamii yako iliyokuzunguka.

By Richard Edward

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

JE NI SAWA KUMSIFIA MWENZI WAKO KWA MARAFIKI ZAKO!!

Richard Edward | 10:24:00 AM | Toa maoni yako hapa!
 JE NI SAWA KUMSIFIA MWENZI WAKO KWA MARAFIKI ZAKO!!
Yapo mambo mengi yanayotokea kila siku katika maisha ya mahusiano, mambo hayo yanawezekana kuwa ni ya lazima kutokea, unayasababisha mwenyewe au unaruhusu yatokee bila ya sababu.

Kutokana na hayo yote, leo nitazungumzia baadhi ya wapenzi wenye tabia za kutoa mambo ya faragha na kuyapeleka kwa mashoga au rafiki zao.

Kila unachokifanya usiku, mchana au asubuhi na mpenzi wako, basi mama au baba wa jirani anafahamu, mkikwaruzana kidogo, ukimnyima mwenzio haki yake ya ndoa, basi mama au baba mwenye nyumba anajua kila kitu kilichotokea.

 Hii sio sawa, hili ni tatizo ni moja ya upungufu mkubwa katika uhusiano, sasa utofauti wenu mkiwa mmevaa na mkiwa watupu uko wapi ikiwa kila kitu unaenda kukianika kwa rafiki zako?

Isikupite Hii: Changamoto Kuu sita (6) Za Mahusiano Ama Ndoa

Unadhani yeye hapendi vitamu na vizuri au raha kama ambazo umekuwa ukimsimulia? Unadhani yeye hapendi raha na ujuzi ndani ya sita kwa sita!

Usitengeneza mazingira ya kumshawishi mtu dhidi ya mpenzi wako, ya chumbani yabaki kuwa ya chumbani na ya sebuleni yawe ya sebuleni, pia ya kijiweni au saluni yaishie huko huko. Usichanganye ya chumbani na sebuleni au saluni kuwa sehemu moja, utakuwa umeharibu sana.

Kama kuna kosa kubwa ambalo ulikuwa hulijui linaweza kukumaliza kwenye uhusiano basi ni mwanaume au mwanamke kuwasimulia rafiki zake kuwa mumewe au mkewe anayaweza mambo fulani au ana upungufu fulani.

Kwanza inashangaza sana unawezaje kusimulia mambo nyeti kiasi hicho, mambo ya faragha ni siri kama ilivyo usalama wa taifa, ndivyo ambavyo unapaswa kuiona kuwa ni sekta nyeti sana.

Kwa kweli inasikitisha kuona kila unachofanyiwa na mpenzi wako unakwenda kuwaambia mashoga zako. Eti, ooooh! Jana bwana’angu kanifanyia hivi, kanigeuza hivi, kiukweli usiku wa jana nimeinjoy sana kwa penzi la mpenzi wangu, nashukuru Mungu nimempata mpenzi anayeyajua mambo, kwa hilo sina shaka kabisa.

Tabia hii ipo kwa pande zote mbili, wanaume kuhadithiana na hata wanawake pia kufanya hivyo, lakini siyo wote. Unakuta kijana yuko kijiweni na washikaji zake kakazana kuwasimulia wenzake, Mwajuma ni mjuzi faragha, anajua kuzungusha nyonga hakuna mfano wake, mwanangu yaani nashindwa namna ya kuelezea wewe elewa mambo anayaweza.


By Richard Edward

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

ASALI TIBA YA MARADHI 27

Richard Edward | 7:16:00 AM | Toa maoni yako hapa!
asali na tiba
 
 Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote.

Warusi na Wafaransa wanafahamika sana katika kufanya utafiti katika maabara kuhusu uwezo wa asali katika tiba mbali.

Baadhi ya vitabu vingine vinavyofahamika kuandikwa na watafiti kuhusu uwezo wa asali katika tiba.

Moja kile cha BEES DON'T GET ARTHRITIS CHA FRED MALONE NA BEE IN BALANCE CHA AMBER ROSE.
Leo tuangalie tiba ya asali na mdalasini na namna ya kuitumia kutibu maradhi mbalimbali(asali tunayoizungumzia hapa ni asali safi mbichi.)

BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA KWA ASALI NA MDALASINI NI KAMA IFUATAVYO:

1.UGONJWA WA VIUNGO/MAUMIVU NA UVIMBE(ARTHRITIS)

-Chukua maji kiasi vuguvugu na ongeza mdalasini (unga kijiko cha chai na asali vijiko 2 vya chakula na kuchua sehemu zenye maumivu)
 

-Vilevile waweza kutengeneza kikombe kimoja cha chai kwa kuweka kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na kuongeza asali vijiko viwili vya chakula na kisha kunywa ikiwa ya moto kutwa mara mbili(asubuhi na jioni)

2.KUKATIKA KWA NYWELE(HAIR LOSS)


-Asali ikichanganywa na mdalasini na mafuta vuguvugu ya olive hutia kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele.
 

-Tumia mchanganyiko huo vuguvugu kwa kupaka na kusugua kichwani na acha kwa dk 15 kisha uoshe.

3.UKUNGU WA MIGUU(FUNGUS)

-Changanya kijiko cha chakula cha asali na vijiko viwili vya chai vya mdalasini na acha kwa muda wa nusu saa kisha safisha .(rudia hivyo mpaka upone)

4.MAAMBUKIZI KWENYE KIBOFU CHA MKOJO(BLADDER INFECTION)

-Changanya maggy ya maji vuguvugu na vijiko2 vya chai vya mdalasini na kijiko1 cha asali huondoa bakteria kwenye kibofu.

5.MAUMIVU YA JINO(TOOTHACHE)

-Changanya sehemu tano za asali na sehemu moja ya mdalasini na dondoshea kwenye jino linalouma hadi maumivu yatakapotoweka.

6.VIDONDA VITOKANAVYO NA MAGONJWA YA KULALA KWA MUDA MREFU(BED SORES)

-Paka saladi iliyochanganywa asali na mdalasini.Vilevile tumia chai ya roseberry nyekundu kwa kuondoa maumivu makali ya canker sores/bed sores.

7.LEHEMU(CHOLESTRAL)


-Changanya asali safi mbichi vijiko2 vya chakula na unga wa mdalasini vijiko2 vya chakula na kikombe cha chai cha maji ya moto na unywe kutwa mara 3

8.MAFUA(COLDS)

-Tumia mchanganyiko wa kijiko 1 cha chakula cha asali vuguvgugu na robo kijiko cha unga wa mdalasini kuondoa chafya na kuvimba koo.

9.UGUMBA(INFERTILITY)

-Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi.Kwa wapenzi. wa jinsia zote wanashauriwa kunywa walau vijiko 2 vya chakula kila siku kabla ya muda wa kulala..Mdalasini imetumika muda mrefu katika dawa za kichina na kihindi kuongeza uwezo wa uzazi kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa
 

-Changanya mdalasini na kiasi cha asali na kufanya mgando (paste)na upake kwenye fizi na meno na kuacha inyonywe na kuingia mwilini taratibu na hii ni kwa akina mama wasio na sababu za kimsingi za kuwakosesha kuzaa.

10.MCHAFUKO WA TUMBO(STOMACH UPSET)


-Asali kwa muda mrefu imetambulika kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo na kichefuchefu.Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali pia hupunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

11.GESI(ACID)

-Kula asali pamoja na mdalasini kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi(acid)huu ni uchunguzi ulio fanywa na Japan na India

12.UGONJWA WA MOYO(HEART DISEASE)
-Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara kwa kupakaa kama jam wakati wa kula mkate wa ngano wenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko 1 cha chakula cha mchanganyiko huo(asali na mdalasini) kila siku

13.SHINIKIZO LA DAMU(H/B/P)

-Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya upata dozi ya mara kwa mara ya asali iliyochanganywa na mdalasini.

14.KINGA YA MWILI(IMMUNE SYSTEM)


-Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja.Utafiti unaonyesha kuwa hazina  kubwa ya vitamini(virutubisho),madini pamoja na mchanganyiko wa mdalasini na asali iondoayo magonjwa na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za damu husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea(virus)na bakteria.

15.UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME(UHANITHI/IMPOTENCE)

-Asali ina historia ndefu ya kuamsha nguvu ya uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji.Asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za mashariki za dunia.Watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali inauwezo wa kupelekea mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo mdalasini.
 

-Katika Afrika na dunia ya kusini mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza nguvu ya kufanya mapenzi.

16.KUTOKUCHAGULIWA KWA CHAKULA(INDIGESTION)

-Kula vijiko 2 vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo huondoa kiungulia na wataalam wanasema asali husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa chakula tumboni na mdalasini unaongeza kasi ya kuchaguliwa kwa chakula.

17.FLU(INFLUENZA)

-Tafiti  moja ya Kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa iliyopo katika asali ni dawa moja asilia ya ajabu ambayo huharibu vimelea(virus)waletao flu.

18.KUONGEZA UMRI WA KUISHI(LONGEVITY)


-Unaweza kuishi hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali.Kutengeneza kinywaji hiki kitamu weka vijiko

4(vikubwa)vya mdalasini na vijiko 4 vya asali,vikombe 3 vya maji na koroga kwa dk 10 kisha kunywa robo kikombe mara 3 au 4 na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.

19.KUONDOA CHUNUSI(PIMPLES)
-Changanya vijiko 3 vikubwa vya asali na kijiko 1 kikubwa cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.Uwezo wa asali wa kuua bakteria unafanya uso kuwa wa kawaida katika muda wa wiki 2.

20.KUUMWA NA WADUDU(WASHA WASHA WENYE SUMU)

-Changanya asali na mdalasini kisha pakaa moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia tena hadi uvimbe uishe.

21.MADHARA YA NGOZI(INFECTIONS)

-Fanya kama ilivyoandikwa namba ishirini hapo juu.

22.KUPUNGUZA UZITO.

-Waweza kufurahia vyakula vyote unavyovipenda kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye nguvu na ladha nzuri kilichojaa vitu muhimu viwili ambavyo ni asali na mdalasini.
 

-Unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika mapishi yako.Vilevile wataalam wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyama nyama nje ya mwili kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko 2 vikubwa vya asali na kijiko 1 cha mdalasini.Rudia mchanganyiko huo kabla ya kulala.Wataalam wamethibitisha kuwa inapunguza hamu ya kula na kuleta joto mwilini.

23.SARATANI(CANCER)

-Utafiti uliofanyika huko Australia na Japan umeonyesha kuwa asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya magonjwa kwa anaetumia madawa ya kutibu saratani.Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua saratani ya mifupa na utumbo ambao walikuwa wanatumia kila siku dozi ya asali na mdalasini walionyesha kupata nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa wanatumia madawa ya kutibu saratani peke yake.Dr.HIROKI OWATA alisema waliwapa mchanganyiko wa asali na mdalasini kijiko kimoja kutwa mara 3 kwa mwezi 1 na wengine waliendelea kama kawaida.

24.KUONDOA UCHOVU(FATIQUE)

-Uko ushahidi kwamba sukari asilia iliyopo katika asali inauwezo wa kuongeza nishati mwilini.Zikitumika ipasavyo sukari hii inaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu.Wataalam wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu kikombe cha maji yaliyonyunyiziwa mdalasini kunywewa masaa mawili baada ya kuamka.Rudia kunywa saa 9 alasiri wakati nishati(nguvu)inapoanza kuisha kufuatia ushauri wa dr.MILSTON ABBOZZA ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa.

25.KUVIMBA NYAYO(SOREFEET)

-Changanya asali na mdalasini katika maji vuguvugu na uchue miguu(nyayo)zilizoathirika baada ya siku ndefu ya kazi au baada ya mazoezi marefu.Rudia kila asubuhi na unawe nyayo kwa maji baridi na vaa viatu.

26. HARUFU MBAYA MDOMONI

-Chukua maji ya vuguvugu changanya na asali na mdalasini kisha sukutua kila asubuhi.Katia Asia ya kusini mashariki watu hula kijiko cha asali na mdalasini ili kuondoa harufu mbaya(halitosis).Wataalam wanaamini uwezo wa kuua bakteria uliopo kwenye asali ndio unaopigana na harufu mbaya toka mdomoni.

27. KUPUNGUA KWA USIKIVU(LOSS OF HEARING)


-Dozi za kila siku za asali na mdalasini hufanya hali ya usikivu kuwa makini kama ilivyogunduliwa na Wagiriki zamani.
-Kutumia mdalasini na asali kutakufanya uonekane kuwa na afya nzuri.
 


By Richard Edward

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

KULA VIFUATAVYO KAMA UNASAMBULIWA NA MAFUA

Richard Edward | 7:15:00 AM | Toa maoni yako hapa!
 Mafua  ni ugonjwa unao-sumbua watu  kila mwaka, hasa yanayo  anza kutokea mabadiliko ya  hali  ya hewa  kutoka msimu wa  kiangazi  kuingia  masika.

Ili  kujikinga  na  ugonjwa  wa  mafua  ni  lazima  mwili uwe  na  kinga  ya  kutosha.

Orodha  ya  vyakula  vifuatavyo  vimeelezwa  kuwa  na  uwezo  mkubwa  wa  kuimarisha  kinga  ya  mwili na  kupambana  na  maambukizi  mengine  kwa  kuwa  na  kiasi  kikubwa  cha  protini  na  virutubisho  vingine.
 

SUPU  YA  KUKU
Supu ya  kuku  wa  kienyeji  inaelezwa  kuwa  na  virutubisho  vinavyo  saidia  kupunguza  utokaji  wa  makamasi.
Supu  ya  kuku Utapata  virutubisho  vingi  zaidi  ukitengeneza kwa  kuchanganya  na  mboga  za  majani. Weka  chumvi  kiasi  kidogo  katika  supu  hiyo.
 

VITUNGUU  SAUMU
Vitunguu  saumu  vina  kirutubisho  aina  ya  ‘ allicin’  ambacho  kina  uwezo  wa  kutoa  kinga  dhidi  ya  magojwa  mbalimbali  ya  kuambukiza.

Vitunguu  Saumu kinatoa  kinga  halikadhalika  kinapunguza   muda  wa  mtu  kuumwa  na  mafua.
 

Tumia  kitunguu  hicho  kwa  kupika  kwenye  chakula  au  kwa  kutafuna  punje.
 

Soma:Jikinge na ondoa harufu mbaya mdomoni

CHAI
Chai  hasa  ya  kijani, ( Green  Tea ) ina  virutubisho  vya  kuimarisha  kinga  ya  mwili .

Utafiti  wa  hivi  karibuni  ulio  fanywa  na  jarida  moja  la  masuala  ya  virutubisho  nchini  Marekani ( Journal Of  the  American College  of  Nutrition )  umeonyesha  kuwa  watu  wanao  tumia  chai  kwa  mpangilio  maalumu, hawasumbuliwi  mara  kwa  mara  na  mafua  pamoja  na  magonjwa  mengine  ya  kuambukiza, huwa  salama  na  mafua  au  siku za  kuumwa  mafua  hupungua  kwa  asilimia  36 ukilinganisha  na  wale wasio  kuwa  na  kinga  imara.

Hata  hivyo, tahadhari  inatolewa  kwa watoto wa  shule kutokupewa  kiasi  kingi  cha  chai kwa  siku.

Unywaji  wa  kikombe  kimoja  kwa  siku  kwa  mototo  wa  shule  siyo   mbaya.

Kwa  mtu mzima, usizidishe   vikombe vitatu  kwa  siku.
Ikumbukwe  kuwa, chai  inapotumika  kwa  wingi  kupita  kiasi, huweza  kusababisha  pia  tatizo  la  kukosa  choo  kwa  muda  mrefu.

Kunywa  kiasi  kwa  afya  yako.

 MACHUNGWA, PILIPILI  KALI

Utafiti  unaonyesha  kwamba, ulaji  wa  vyakula  vyenye  Vitamin  C  kwa wingi  kila  siku  husaidia  kuondoa  au  kuzuia  ugonjwa  wa  mafua.

Machungwa
Miongoni  mwa  vyakula  vyenye  kiwango  kikubwa  cha  Vitamin  C ni  pamoja  na  machungwa, mboga  za  majani  aina  ya  Brokoli  na  pilipili kali.

Pilipili Kali
Ili  kupata  kiasi kingi  cha  Vitamin C, inashauriwa  machungwa  yaliwe   pamoja  na  nyama  zake  za  ndani  au  kunywa  juisi  yake.
 

ASALI
Kama  inavyo  julikana, asali  ni  tiba  ya  matatizo  mengi  ya  kiafya, miongoni  mwa  hayo  ni  pamoja  na  mafua.
Asali  inasaidia  kuondoa  kikohozi  na  muwasho  kwenye  koo.  Halikadhalika, asali  inaweza  kutumiwa  na  watoto wadogo  kama  dawa.

Watoto  wanao  ruhusiwa kutumia  asali  kama  tiba  ni  wa  umri  wa  kati  ya  miaka  2  hadi  5.
 

Hawa  dozi  yao  ni  nusu  kijiko  kidogo  cha  asali, wenye umri  wa  miaka  6 hadi  11  wapewe  kijiko  kimoja  kidogo  na  wenye  umri  wa  kuanzia   miaka  12  hadi  18, wapewe  vijiko  vidogo  viwili  vya  asali  wakati  wa  kulala.

 MTINDI
Kutokana  na  kiwango kikubwa  cha  protini  ilicho nacho, Mtindi  ni  chakula  kingine  kinachofaa  kuliwa  na  mtu  mwenye  mafua  ili  kupunguza  siku  za  kusumbuliwa  na  ugonjwa  wa  kukohoa.


Soma:Watu wanene ndio wengi duniani

CHOKOLETI  NYEUSI
Wataalamu  wanakubaliana  kuwa, ulaji  wa  ‘chocolate’ nyeusi ( Dark  Chocolate ), huimarisha  kinga  ya  mwili, hivyo  inapoliwa  na  mgonjwa  wa  mafua, huweza  kumpa  ahueni  mgonjwa  kwa  namna  moja   ama  nyingine, na  pia  huwa  kinga  kwa  magonjwa  mengine.
 

PWEZA
Samaki  aina  ya  pweza  wana virutubisho  vingi  vya  kuongeza  kinga ya  mwili  yenye  uwezo  wa  kupambana  na  bacteria  pamoja  na  virusi  vya  mafua.
 

Kiasi  kidogo  cha  pweza, awe  wa  kukaangwa  au  kuchemshwa  kama  supu,  anafaa  kuliwa  mara  kwa  mara  kukmarisha  kinga  ya  mwili.
 

VIAZI  VITAMU
Kirutubisho  aina   ‘ Beta carotene’  huimarisha  kinga  ya  mwili.

Kirutubisho  hicho  huwa  ni  muhimu  kwa  ustawi  na  uimarishaji  wa   kinga  mwilini  na  kinapatikana  kwa wingi  kwenye  viazi  vitamu na  vyakula  vingine  kama  vile  karoti, maboga  na  mayai ( kiini)
 

Kwa  ujumla , suala  la  kuimarisha   kinga  ya  mwili  ni  muhimu  kwa  afya  zetu.

Ulaji  wa  vyakula  vilivyo  tajwa  hapo  juu  na  vingine, unatakiwa  kuwa  ni wa  mara  kwa  mara  kama  siyo  wa  kudumu, kwa sababu  mwili  unapokosa  kinga  imara, ni  rahisi  kushambuliwa  na  maradhi  ya  kuambukizwa.


By Richard Edward

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.
 
Content By Chief Hope | Facebook | Twitter | Copyright ©2016 TIM HEAVEN