Saturday, April 12, 2014

RUNGU LA YESU NDANI YA MISHENI MPYA! NI IPI? NA WAPI? SOMA HAPA!

Chief Hope | 9:17:00 PM |

Kwa mara Nyingine Tena RUNGU LA YESU  anaondoka unyamwezini kwenda kula pasaka, Misheni yake inaambatana na mambo mengi sana.
Jambo la kwanza atakuwa na semina katika kanisa la FPCT Bomba Mzinga kuanzia Jumatano hii ya Tarehe 16/4/2014 Mpaka Jumapili ya Tarehe 20/4/2014 Ambayo itakuwa ni siku ya Pasaka, RUNGU LA YESU atakuwa akifundisha Neno La Mungu Kanisani hapo.
Na jioni ya Pasaka kutakuwa na tamasha la YESU OKOA MITAA, RUNGU LA YESU anamewaomba wakazi wa Tabora kujitokeza kwa wingi kwenye Semina hiyo na Jumapili maana  ambayo itakuwa ni kilele Cha YESU OKOA MITAA.
Kanisa la FPCT Bomba Mzinga lipo pale Mjini Tabora linaloongozwa na Mchungaji DAVID AMON.
RUNGU LA YESU pia anawatakia utulivu katika kipindi hiki cha pasaka.
YESU OKOA MITAA, KILA KONA YA MTAA!  

5 comments:

 1. big up bro! YESU OKOA MITAA

  ReplyDelete
 2. Na iwe hivyo yetu maombi tu kazi ya Injili izidi songa.
  Asante #TimHeaven kwa kutuhabarisha.
  #YOM_Tz.

  ReplyDelete
 3. Kwa hiyo tamasha la pasaka uwanja wa taifa hatakuwepo?

  ReplyDelete
 4. Hapana rafiki hii haiingiliani na tamasha la Pasaka la uwanja wa taifa!
  Rapper Rungu la Yesu atafanya yake ndani ya mkoa wa Tabora.

  ReplyDelete
 5. Nilisikia lumaz kwamba katika tamasha la pasaka kutakuwa na wanamuziki wa kizazi kipya pia ni ukweli au?

  ReplyDelete

 
Content By Chief Hope | Facebook | Twitter | Copyright ©2016 TIM HEAVEN