• Isikupite Hii

  December 9, 2014

  YUSUFU NA RUNGU LA YESU - TUNZA IMANI NA USIKATE TAMAA!

                                             
  Ni Miaka Mingi Sasa Tangu Tufamiane Na Rungu La Yesu, Na Leo Tunahaya Ya Kusema Juu Ya Rungu La Yesu. Mbali Na Vyeo Vingine Alivyonavyo Rungu La Yesu Akiwa Ni Mwanzilishi Wa YOM Project 

  Rungu La Yesu Ni Moja Kati Ya Watu Wachache Wasiokuwa Na Roho Ya Uoga Kama 2 Timotheo 1:7 Inavyosema Na Pia Ni Rungu La Yesu Mtu Asie Kata Tamaa Katika Hali Yoyote Hile.
               
  Tangu Miaka Hiyo Ya Zamani Ambapo Huduma Hii Ya Gospel Hip Hop Ilipokuwa Ikipingwa Na Watu Wengi Sana Wenye Vyeo Na Wasio Kuwa Navyo Kwa Sababu Wengi  Waliona Huduma Hii Kama Ni Uhuni Na Ushetani.

  Rungu La Yesu Amepitia Hali Ya Kutaliwa Na Watu Mbali Mbali Kwa Sababu Ya Mtazamo Ambao Watu Hao Waliokuwa Nao! Ametukanwa Na Kuhambiwa Mambo Yasiofaa. 

  Wengine Walikata Tamaa Na Kuachana Na Huduma Hii Ya Gospel Hip Hop Lakini Rungu La Yesu Haku Kata Tamaa Na Wala Hakuicha Imani Aliilinda Na Kuitunza Imani Yake. Na Leo Rungu La Yesu Ni Moja Kati Ya Waimbaji Wakubwa Wa Gospel Hip Hop Hapa East Africa.
             
  Hii Inaturudisha Nyuma Kidogo Na Kutukumbusha Juu Ya Kijana Moja Maarufu Sana Katika Agano La Kale "Yusufu A.K.A Baba Ndoto". 

  Yusufu Alikuwa  Ni Kijana Mwenye Ndoto Nyingi Na Kubwa, Hali Na Mazingira Aliopitia Yusufu Zilikuwa Zikipingana Na Ndoto Zake. Aliuzwa Utumwani Kwa Potifa, Kisha Akafungwa Gerezani But Yusufu Hakuwai Kukata Tamaa, Aliitunza Imani Na Akasimamia Haki.Na Wote Tunaujua Mwisho Yusufu, Alikuwa Wazima Mkuu Wa Misri Enzi Za Farao.

         
                 Ndugu Mpendwa Najua Unamaono, Ndoto, Mipango Na Mambo Mbalimbali Na Labda Unapitia Hali Ngumu And You Feel Like Giving Up. Siku Ya Leo Nasimama Na Kukutia Moyo Kwammba Mungu Yuko Na Wewe, Unachotakiwa Kufanya Ni Kuitunza Imani Ulio Nayo Na Kutokukata Tamaa!

  BY #TIM HEAVEN