• Isikupite Hii

  January 31, 2015

  VIJANA WA YESU OKOA MITAA KUACHIA WIMBO MPYA "WARAKA WA YOM"!


  Vijana Wa Yesu Okoa Mitaa Wamekuwa Kimya Kwa Mda Mrefu Sana Hadi Watu Wengine Wameanza Kuzusha Maneno Kwamba Harakati Za Vijana Hao Zimekufa. Hapana Si Kweli Kwamba Harakati Za Vijana Hao Zimekufa Ndo Kwanza Harakati Za Yesu Okoa Mitaa Zimeanza. 

  Vijana Hao Wa (YOM) Wametangaza Kuachia Wimbo Mpya Unaokwenda Kwa Jina La "WARAKA WA YOM". Wimbo Huo Utaachiwa Rasmi Tarehe 6/2/2015, Mida Ya Saa 8:00 Mchana, Praise Power Radio Katika Kipindi Cha Sifa Moto. Baada Ya Hapo Wimbo Huo Utaanza Kusikika Katika Vituo Mbali Mbali Vya Radio Hapa Nchini. Lakini Pia Utaweza Kuudownload Wimbo Hua Hapa Hapa Kwa Blog Hii Na Mitandao Mengine Mingi. 

  Rungu La Yesu Ambae Ni Kiongozi Wa Harakati Hizo Amesema Kwamba "This Is Just The Beginning, Kazi Nyingi Zaidi Na Kali Zinakuja". Aliendelea Kusema "Lengo Sio Kushinda Ama Kujinyakulia Utukufu Bali Kuhakikisha Injili Ya Kristo Inasambaa Katika Kila Kona Ya Mtaa Na Yesu Kristo Anainuliwa Juu Zaidi".

  Lengo Kuu La Wimbo Huo "WARAKA WA YOM" Ni Kuwaelezea Watu Juu Ya MUNGU, Ubaya Wa Dhambi Na Kuwakumbusha Yesu Kristo Ndio Njia Pekee Na Kwake Yote Wanawezekana.  

  Mimi Binafsi Nimepata Nafasi Ya Kusikiza Demo Ya Wimbo Huo Kiukweli Ni Wimbo Mkali Sana. Ndani Ya Wimbo Huo Mpya "WARAKA WA YOM" Utapata Kuwasikiliza Vijana Wenye Uwezo Mkubwa Wa Kuflow Lakini Pia Uwezo Mkubwa Wa Uandishi Wa Mashairi Yanayompa Mungu Utukufu Na Yanayotujenga Kimwili Na Kiroho Pia. Na Vijana Hao Ni Rungu La Yesu, SirMbezi, Eka Injili, Chief Hope, Magele Winner, Amani Shabani, Morefire Na George Maige.