• Isikupite Hii

  February 26, 2015

  MFAHAMU MWANADADA EUNICE MWAIPOPO NA HUDUMA YAKE.


  Eunice Mwaipopo "Nimezaliwa Mbeya, Mimi ni muimbaji wa muziki wa injili. Nilianza kuimba nikiwa mdogo sana, Nikiwa darasa la kwanza. 

  Napenda sana kuimba kwa sababu huwa nafarijika sana, na ninapo imba huwa nahisi kuwa karibu na Mungu. Mimi hupenda kuwakilisha maombi na shukurani zangu kwa Mungu kwa njia ya nyimbo (kuimba). 

  Niko kwenye maandalizi na hivi karibuni nitaachia Album yangu ya kwanza. 

  Navutiwa sana na waimbaji wa southAfrica pamoja na waimbaji wa Marekani huwa napenda kuwa sikiliza wanavyoimba na kujaribu kuimba kama wao. Safari yangu ya uimbaji naweza kusema imekua salama maana huwa ninaimba kanisa mda mwingi, Changamoto ni kukosa mazoezi yanayoweza kunifanya niwe muimbaji bora zaidi.

  Kinachonifuraisha kwenye muziki wa injili ni jinsi waimbaji wanavyo present nyimbo zao, wanavyoweka jitiada na  kuhakikisha ujumbe unawafikia wahusika, wengine ufunga na kuomba, wengine husoma sana neno".

  Download Wimbo Mpya Ambao Mwanadada Eunice Mwaipopo kashirikishwa.