• Isikupite Hii

  February 26, 2015

  MARTHA MWAIPAJA ATANGAZA KUSAPOTI WAIMBAJI.


    "Shalom!!!  Sikuanzia Hapa nilipo bali nilianzia chini sana na MUNGU Kunipa kibali cha kufika hapa nilipo.. Leo nina Kitu cha kufanya kwa ajili ya Watumishi wanaomuimbia Mungu Ambao ndio wanaanza au kwa Muda Mrefu wamekuwa wakifanya Huduma ya Uimbaji bila Mafanikio ya Uandaaji Mzuri Wa Kazi ZAO.
  Nahitaji kusaidia watu watatu (3) ambao ni waimbaji kufanya Video zao kwa kuwachangia Asilimia 25 ya Gharama ya Video kwa Kila Mmoja. 
  VIGEZO..
  1.Kusudi la kuimba kwako liwe kwa ajili ya Mungu na si kwa Masilahi fulani
  2.Uwe ni muimbaji wa nyimbo za Injili
  3.Uwe na Audio kamili tayari
  4.Uwe ni mtu ambaye upo tayari kufanya Video Kuanzia Sasa maana Project hii nahitaji iishe mapema wa kipindi hiki ambacho Mungu Amekusudia
  5.Uwe ni mtu ambaye unaweza kuja Dar maana Kiasi cha Pesa nitakachotoa nitakitoa kwa muhusika kwa kuonana naye na kuzungumza naye kuhusu safari yake ya Uimbaji.
  Asanteni Sana Na Mungu Awabariki Sana..
  N.B- TANGAZO HILI LIMFIKIE HATA AMBAYE SI RAFIKI YANGU FACEBOOK ILI NIPATE KUSIKIA AUDIO NYINGI ZAIDI PENGINE MUNGU ANAWEZA NIFUNULIA KUFANYA KINGINE ZAIDI JUU YA MUIMBAJI HUYO.
  SHARE NA WATUMISHI WENGINE" Alisema Martha Mwaipaja Kupitia Fan Page Yake Ya Facebook.