• Isikupite Hii

  March 10, 2015

  RAIS MAGUFULI STORY NA UTANI KABLA YA URAIS. (+VIDEO)


  Kuna wakati unajikuta unaelekea njia ambayo hujaipanga kwenye maisha yako lakini kumbe Mungu alikupangia huko siku nyingi tu, jina la Dk. John Pombe Magufuli huenda halikupewa nafasi kubwa sana na watu wengi kwenye kumtarajia kuwa Rais mpya wa Tanzania hasa ukiiangalia list ya makada 38 wa CCM walioingia kwenye mchakato wa kugombea Urais 2015, mwisho wa siku akapita yeye na akapata Urais !!

  Hata wakati amechukua fomu ya kugombea Urais hakuwa na mbwembwe wala kujitangaza lakini mwisho wa siku ndio akawa Rais, sasa leo nimepata hii video kutoka kwa mtoa habari Subi Nukta inayoonesha Rais Magufuli akiwa kwenye stori tu na watu wengine enzi hizo akiwa Waziri wa ujenzi, stori zao walikuwa wanagusia ishu ya madini ya Tanzania… mmoja akamchomekea kwamba achukue fomu ya Urais ili abane uchakachuaji wa madini… unajua alijibu nini ?! Cheki hii video ya dakika 2:45.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.