• Isikupite Hii

  March 31, 2015

  MWANADADA HUYU ADAI KUPEWA UJUMBE NA RAIS GADDAFI NA WHITNEY HOUSTON WAKIWA KUZIMU.


  Mwanamke mmoja kutoka Sierra Leon aitwaye Linda Kumba Isatu Ngaujah anayedai kwamba alikufa mwezi February 15 mwaka 2013 na kupelekwa moja kwa moja kuzimu ambako alikutana na ibilisi na kudai alipatiwa ujumbe kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Libya marehemu Gaddafi, mwimbaji Whitney Houston pamoja na Rais wa Guinea Lansana Conte ambao kwa madai wapo kuzimu


  Katika ushuhuda wake amesema


  "Yesu alimtoa mwanaume mmoja kutoka kwenye moto na kujitambulisha kwangu kwamba yeye ni Gaddafi (huwezi kunitambua kwasababu moto umeniharibu, alisema), Gaddafi akamwambia "Mimi ni Gaddafi Rais wa zamani wa Libya, waambie Walibya wamwabudu Yesu, waambie wamwamini Yesu, akasema "Ah Yesu nionee huruma, sijawahi kujua njia ya kweli, nisamehe, Gaddafi alisema asingependa hata watu waliomuua duniani nao waende kuzimu alipo, waambie watu wangu wamwamini Yesu ni njia ya kweli na uzima" alisema Gaddafi


  Nikamuona Rais mwingine ambaye ni mstaafu kutoka Guinea, kwanini Yesu amenionyesha hawa watu, ni kwasababu amenipa ujumbe kwa watu wa Sierra Leone, alisema "Waambie watu wangu wamwamini na kumfuata Yesu na kuachana na kuamini mizimu na kutaka watu waache walichokuwa wakikiabudu na kukifuata, ila wakiharibu na kumfuata Yesu" alisema Rais huyo akiwa kuzimu.


  Nilimuona nabii kiongozi wa kanisa la Burning Bush Emmanuel Mani, enzi za uhai wake mwanaume huyu alisema atakufa lakini siku ya tatu atafufuka. N alipokufa waliuchukua mwili wake na kuuhifadhi kwenye chumba cha maiti, kwasababu waumini wake walisema hawatamzika, baada ya siku tatu hakufufuka, alikuwa chumba cha maiti kwa mwezi mzima mpaka wafanyakazi wa chumba cha maiti waliwataka kwenda kuchukua mwili wao


  Nilimuona mwanamke mmoja, mwanamuziki niliyempenda sana siku zote nilikuwa nasikiliza muziki wake wakati nikiwa duniani Whitney Houston. Aliniambia "Mwambie mama yangu ampeleke binti yangu kanisani, pesa zote nilizoziacha zitumike katika kusapoti kazi ya Mungu, waambie wasapoti kazi ya Yesu, waambie wasapoti huduma takatifu, waambie wasapoti kazi ya Mungu. Waambie wasapoti Wakristo - Wakristo wa kweli.


  Niliwaona wazazi wangu kuzimu, mama na baba yangu hata bibi yangu aliyekufa mwezi january mwaka huu (sipendi kuzungumza kuhusu wao) ni maumivu makali. Alisema mwanadada huyo katika ushuhuda wake kama ulivyoandikwa kwenye blog ya Poko.


  Source: GospelKitaa.