Wednesday, May 20, 2015

MISTARI 10 YA BIBLIA ITAKAYO KUFARIJI NYAKATI ZA UPWEKE.

Chief Hope | 6:25:00 PM |
Mistari hii 10 ya Biblia inatukumbusha kwamba hatuko peke yetu. Daima Mungu yu pamoja nasi. Pokea nguvu kupitia neno la Mungu na umimine moyo wako kwake yeye, anaye yajua mahitaji yako yote na yeye hujibu pale unapolitia jina lake.

Yohana 14:18 
Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

Yoshua 1:5
Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha. 


Isaya 41:10
Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Zaburi 27:10
Baba yangu na mama yangu wameniacha, Bali Bwana atanikaribisha kwake.

Kumbukumbu La Torati 31:8
Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike. 

Zaburi 62:8
Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu. 

1 Yohana 4:13
Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake. 

Zaburi 94:17
Kama Bwana asingalikuwa msaada wangu, Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya. 

Zaburi 145:18
Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu. 


Yeremia 29:11
Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. 

By Chief Hope

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk. 

0 comments:

 
Content By Chief Hope | Facebook | Twitter | Copyright ©2016 TIM HEAVEN