• Isikupite Hii

  July 27, 2015

  EXCLUSIVE: CHURCH-BOY&CHURCH-GIRL KUZINDULIWA RASMI DAR ES SALAAM. TAREHE 7 AUGUST 2015.

                                 

  Kwa mara ya kwanza ChurchBoyChurchGirl inazinduliwa Dar-es salaam pale Word Alive Sinza. Tarehe 7 Mwezi 8, Kuanzia Saa 3:00 Usiku Hadi Saa 11:00 Asubuhi. Usikose!

  Churchboy na ChurchGirl ni mpango wenye lengo la kuwasaidia vijana, kumjua Mungu na kuwakumbusha kuwa kuokoka sio ushamba, kuwaepusha vijana na matumizi ya madawa ya kulevya, maadili mabaya na kila aina ya uchafu miongoni mwa jamii zao. 

  Church Boy na Church Girl inatumia mbinu za kipekee za kueneza habari njema za Yesu Kristo kwa vijana wa wakati wetu, lakini pia kuwatia moyo wale waliozisikia hizo habari wakaamua kuokoka lakini kuna wakati wanahisi walikosea kufanya hivyo.

  Pia kuna mambo mengine ya kijamii yanafanywa chini ya mpango huu kama kushauri na kufundisha vijana kuhusu mahusiano sahihi, kujipanga kimaisha, kuwatia moyo vijana wengine kwa kutumia vijana waliookoka ambao wanafanya mambo mbali mbali katika jamii. kusaidia wenye shida(charity), pia kusaidia vijana kukuza vipaji vyao katika kumtumikia Mungu.

  Church Boy  Church Girl ilianzishwa kama zawadi maalum kwa kila kijana kuwawekea hamu na shauku ya kuishi maisha ya utakatifu na yenye mafanikio katika njia ya Kikristo.