• Isikupite Hii

  September 8, 2015

  DOWNLOAD WIMBO: NAPOKEA KWAKO - JANET OTIENO FT CHRISTINA SHUSHO.

  Download wimbo toka kwa Janet Otieno na Christina Shusho "Napokea Kwako"

  Lyrics

  Maisha magumu sana nimepitia 
  Nikajaribu kutafuta msaada sikupata 
  Nikaendea wanadamu mwisho wakanidharaume) 
  Kumbe msaada wa mwanadamu unatoka kwa Mungu 
  Nilijua ya kuwa wenye haki ya kubarikiwa\ 
  Kumbe baraka ni haki ya kila mmoja 
  Nibebadili wazo langu namwelekea Mungu 
  Kwake msaada wangu unapatikana 
  Msaada wa mwanadamu ni wa muda mfupi 
  Nami zamu yangu wa kubarikiwa ee 

  Chorus: 
  Wakati huu wa kubarikiwa 
  Zamu ni yangu, sasa kupokea(\ 
  Nimechoshwa, na shida za dunia 
  Napokea kwako, Ee Bwana kwako x2 
  Napokea kwako, Yesu napokea kwako 
  Napokea kwako, Baba napokea kwako 

  Nimeamua kwenda zaidi na zaidi 
  Nimejipanga hadi nione matunda yake 
  Yale Mungu amewekeza ndani yangu 
  Najua Mungu yuko kazini kunikamilisha 
  Akisema nimebarikiwa, nimebarikiwa tu 
  Hata ukipinga wewe leo mimi nimebarikiwa tu 
  Mlima gani kuu sana usioung’oa? 
  Jaribu gani gumu sana usiloliweza? 
  Chozi gani zito kwako usilolifuta? 
  Ombi gani kubwa sana usilolijibu? 

  (Chorus)