• Isikupite Hii

  SOMA MAKALA, HABARI MBALI MBALI NA MUZIKI WA INJILI TZ

  November 27, 2015

  SABABU ZA UMASKINI AFRIKA - 'WORLD BANK'.


  Sera mbovu, rushwa, migogoro, kukosekana kwa uwazi ni miongoni mwa vyanzo vya umaskini katika nchi za Afrika, imeelezwa.

  Akisoma ripoti ya hali ya umaskini katika nchi tano za Afrika jana, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Tawi la Afrika, Makhter Diop alisema uchumi wa Afrika umekuwa kutoka asilimia 21, mwaka 1990 hadi kufikia asilimia 56, mwaka huu.

  Hata hivyo, imeelezwa kuwa licha ya kukua kwa uchumi huo bado nchi nyingi za Afrika hazina huduma bora katika sekta za afya, elimu na miundombinu kama umeme.

  Ripoti hiyo ilieleza kuwa pamoja na nchi hizo kuweka nguvu kubwa katika sekta ya elimu, afya na kilimo, bado miundombinu ya shule haikidhi mahitaji huku elimu inayotolewa ikiwa ni ya kiwango cha chini.

  “Kwa upande wa sekta ya umeme na kilimo bado kuna changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika, kwenye kilimo nako hakuna mipango thabiti ya jinsi gani mkulima anaweza kunufaika nacho licha ya kuwa ndiyo sekta muhimu katika kukuza uchumi wa nchi pamoja na umeme,” imesema ripoti hiyo.

  Akizungumza katika mdahalo huo, Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Cosmas Kamugisha alitoa suluhisho la umaskini ni kwa Serikali na wananchi kufahamu maana ya dhana ya umaskini.

  “Tunaweza kuilaumu Serikali na sera za nchi husika kutosimamiwa. Kinachohitajika zaidi ni watu kujitambua na kuelewa nini chanzo cha umaskini katika nchi yao na nini maana ya umaskini,” alisema Profesa Kamugisha.

  Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tawi la Dar es Salaam, Profesa Prosper Ngowi alisema sera za nchi siyo rafiki kwa wananchi maskini na nyingi zipo kama mapambo huku wanaotakiwa kuzitekeleza hawafanyi kama inavyokusudiwa.

  Mwakilishi wa WB nchini Tanzania, Bella Bird alisema taasisi hiyo inahitaji kufanya mbinu mbadala ya kutoa elimu kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa kuweka mijadala mbalimbali ya kuwaelimisha wananchi juu ya kuutambua umaskini na njia za kuondokana nao.

  “Tukiangalia hapa Tanzania pamoja na kwamba uchumi na pato la Taifa limepanda kwa asilimia 7.9, bado hali ya maisha ya wananchi ni magumu,” alisema