• Isikupite Hii

  December 12, 2015

  EVENT: THE BORN WINNERS KUZINDUA ALBUM YAO JUMAPILI HII.


  Kundi mahiri la muziki wa Injili nchini Tanzania The born Winners Gospel Movement, Jumapili hii ya tarehe 13/12/2013 watazindua album yao ya kwanza ya DVD waliyoipa jina la Kigeugeu.

  Uzinduzi huo utafanyika katika kanisa la CAG Chuo cha manabii kwa mchungaji Imelda Maboya Ubungo maziwa kuanzia saa nane kamili mchana na kuendelea.

  Hakutakuwa na kiingilio kwenye tamasha hilo, na kwa wanaotaka kazi zao zitapatikana siku hiyo kwa Tsh.10,000/= tu. Waimbaji watakaowasindikiza ni kama Rungu la Yesu, Peter Banzi, Beatrice William, Neema Lyimo n.k.

  TAZAMA VIDEO YA KIGEUGEU HAPA