• Isikupite Hii

  SOMA MAKALA, HABARI MBALI MBALI NA MUZIKI WA INJILI TZ

  December 31, 2015

  JINSI YA KUMKUZA NA KUMLEA MTOTO MWENYE FURAHA.

  Mambo ya kuzingatia ili kumlea mtoto akue akiwa mwenye furaha

  1. Mpe mototo wako muda na uhuru wa kucheza
  Usipende kumpa mtoto wako ratiba ngumu iliyo jaa shuhuli za kufanya na majukumu ya kumfanya awebize wakati wote ukidhani ndo jinsi bora ya kumlea mtoto anayewajibika, Hapana!! Mtoto anayepewa ratiba chache na inayoruhusu muda wa uhuru binafsi huweza kuonyesha vitu anavyovipendelea na vile asivyovipenda, wazazi wengi hupata ugumu kujua vipaji vya watoto wao kwasababu ratiba zao kuanzia wakitoka shule zimejaa vitu ambavyo wazazi wamewapangia sio vitu ambavyo watoto wanavibuni wenyewe huku wakipewa msaada pale wanapohitaji. Sio kitu chema wazazi kulaazimisha watoto wao kufanya au kujua vile vitu ambavyo vi vipaji vya wazazi, kama mtoto atajua mwenyewe na kutamani basi haina shida lakini sio kulazimishwa au kushawishiwa.

  2. Jali sana usingizi, mazoezi na chakula
  Wakati wote wazazitukumbuke kuwa watoto wanapo lala ndio mchakato wa makuzi bora kiakili, kihisia na kimwili unapofanyika. Watoto pia wanatakiwa kufundishwa kutoona mazoezi kama jambo la anasa, hamu na kupenda kushiriki mazoezi ya viungo kuwe kitu cha kawaida kwao, hii itawasaidia sana katika makuzi ya kimwili na kuwaepusha na magonjwa yasiyoyalazima. Mazoezi huwapa ujasiri watoto wakiwa bado wadogo, kwahiyo kama mzazi unapenda kufanya mazoezi basi penda kumshirikisha mwanao hatakama sio kushiriki kiutendaji basi hata kuangalia na kumuelewesha kinachojiri. Kumbuka kumruhusu mtoto kuwa na muda wa kucheza kwasababu katika kucheza ndiko mazoezi ya viungo kwa watoto hufanyika. Hapa nazungumzia kucheza na sio kucheza kucheza.

  3. Usiyachukue matatizo yao
  Baadhi ya wazazi hupenda kuwasaidia watoto wao katika kilakitu, hata katika vile ambavyo watoto hao wangeweza kuvifanya wenyewe. Hata kama maranyingine inaonekana ni kitu kigumu basi waache wajaribu kwanza kwa njia zao wakipata shida taratibu watajifunza kuomba msaada (huku nako ni kujifunza), maranyingine utashangaa wanabuni njia ta kutatua tatizo hilo wao wenyewe na jambo linafanikiwa, mbinu hizi ni vema zianze watoto wakiwa wadogo kwasababu zinawasaidia sana hata katika maisha yao ya baadae. Pale unapokutana na watu wazima ambao hawawezi kuvumilia mara wanapokutana na matatizo madogo tu ujue hawakufunzwa jinsi ya kukabiliana na matatizo yao wenyewe, walitegemea msaada hata katika kitu kidogo. Kumbuka kuwa uwezo wa kuyashuhulikia matatizo na kuyatatua huanza tukiwa bado wadogo.
  Jifunze kuziangalia changamoto za mtoto wako kama zawadi itakayomfanya ajifunze zaidi mbinu na ujuzi mpya. Changamoto hizi zitamfundisha kuwa mvumilivu na mstahimilivu. Zinamfundisha pia jinsi ya kuchukuliana na mazingira.

  4. Check in “Jifunze kuingia kwenye maisha yao mara kwa mara”
  Kama mzazi jifunze na jitahidi kuingia mara kwa mara kwenye maisha ya watoto wako. Usiwe mbali nao kihisia, lugha yako iwe inayoruhusu wao kujiachia kwako katika yote yanayowahusu. Tafuta sana kujua toka kwao, kwa mfano; uliza, “naonakama una huzuni leo vipi?” “hembu niambie shule yako ya jumapili ilikuwaje, ,lifundishwa nini?” Ikiwa atakukataa au kutokukubali katika jitiada zako zakuingia katika maisha yake basi jaribu tena baadae, usichoke haraka kumweka karibu.

  5. Ruhusu hisia zao
  Sio tu kwamba tunataka watoto wetu wawe na furaha bali pia tunatamani wafanye mambo kwa furaha pia, inasikitisha sana kuona mtoto wako analia na kugaragara sehemu wakati wenzake wote wana furaha, sasa famu kwamba suala hapa sio kumwambia acheke bali ni kushuhulikia kile kinachomfanya asionyeshe furaha. Mfundishe mtoto wako kuzigundua hisia zake na kuzielezea kwa maneno, kwa mfano; “Sijafurahi kwa sababu sijabembea mara ya pili kama wenzangu”. Mfundishe mtoto wako kufahamu kuwa ni sawa na nihaki yake kukasirika na sio dhambi wala kosa kwahiyo asiogope mradi tu hasira hizo ziwe zina maelezo bayana na yenye mantiki. Mtoto anapoweza kuzishuhulikia hisia ngumu itamsaidia kuwa na furaha ya kudumu katika maisha yake. Na Dr. Chris Mauki.

  By Chief Hope

   Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.