Friday, May 13, 2016

UNAMTAMBUAJE RAFIKI MWENYE DALILI ZA KUJA KUWA ADUI. (SOMA HAPA)

Chief Hope | 7:55:00 AM | |
Rafiki anaweza kuja kuwa adui au msaliti kwenye mambo mengi yakiwemo
• Kwenye mapenzi
• Kwenye biashara
• Kwenye kupata nafasi kazini
• Kwenye mahusiano na marafiki zenu
• Kwenye mikataba au tenda

Soma: Sababu 5 Za Mikwaruzo Katika Maisha.

Dalili/Mazingira
• Unasikia au unagundua anakusema vibaya kwa wengine, tofauti na akiwa na wewe
• Unahisi au unagundua anakupinga au kukuonea wivu kwenye mambo fulani
• Unahisi au kugundua nia yake ya kutamani kupata zaidi yako
• Unahisi au kugundua kuwa ushauri anaokupa sio wa kukusaidia bali wa kukukwamisha huko mbeleni
Unafanyaje?
• Usimwamini sana mtu wa namna hii
• Usijiachilie na kuwa wazi sana kwa mtu huyu
• Pima ushauri wake na ikiwezekana uliza mtu mwingine pia.

Bora nusu shari kuliko shari kamili – Chris Mauki

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

0 comments:

 
Content By Chief Hope | Facebook | Twitter | Copyright ©2016 TIM HEAVEN