• Isikupite Hii

  SOMA MAKALA, HABARI MBALI MBALI NA MUZIKI WA INJILI TZ

  May 28, 2016

  DALILI 9 ZA RAFIKI, MPENZI AU MCHUMBA ALIYEKUCHOKA.

  1. Anapunguza mawasiliano siku hadi siku. Ni tofauti ukilinganisha ukaribu wa mawasiliano katika kipindi cha awali, mwanzoni alikua moto kwa kipindi hiki utamuona amepoa kama barafu.
  2. Hataki ama anakwepa kuonana na wewe mara kwa mara ukilinganisha na zamani. (ubize ambao zamani hakuwa nao)
  3. Mkiwa wote hachangamki kama zamani.
  4. Atakutafuta akiwa na shida ya pesa ama kitu flani.

  Soma: Tabia 8 Ambazo Huwafanya Wanawake Wengi Washindwe Kuingia Katika Ndoa.

  5. Hujibu kwa ukali mnapojadili jambo na huwa hapendi kurudia jibu lake.
  6. Huwa hajiamini. Hasa sms inapoingia au simu ikipigwa mkiwa wote lazima apepese macho na kukosa amani, kwani simu yake imejaa majanga.
  7. Hataki umuulizie maswali mengi juu ya jambo fulani.
  8. Neno tuachane huwa jirani mdomoni mwake.
  9. Anaanza kukuweka mbali na rafiki ama ndugu zake.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

  Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.