• Isikupite Hii

  February 1, 2016

  MADHARA YA MAZOEA  http://timheaven.blogspot.com/
  1. Mazoea huleta dharau

  Yeyote aliyekujua ukiwa mtoto mdogo hatakuheshimu ukiwa mkubwa.Ni methali ya kiarabu,Kwa ufupi mazoea huleta dharau.

  Mazoea huzaa hata wivu.

  Wagiriki au Wayunani wa zamani walizungumzia mtu mwenye shamba la ngano lenye ukamilifu.Watu walilistaajabia shamba lake.Mabua yote yalikuwa na urefu sawa.Walipo muuliza nni namna ganimabua yote ya ngano yalikuwa na urefu sawa alijibu,"Rahisi.Kila mbeguinayotokeza kichwa chake kuzidi nyingine. nakata kichwa"

  Kuna watu ambao wakimuona mwenzake kijijini ama kazini anainuka kimafanikio wanamvuta chini wanataka wote wawe watu wakawaida yaani wawe sawa.

  Yesu aliheshimika Yerusalemu kwa vile akiwa na umri wa miaka 12 aliwastajabisha walimu hekaluni akiuliza maswali ya nguvu.Yesu aliheshimiwa sana kana alipobadili maji kuwa divai.Lakini Nazareti Yesu alikuwa Yesu.

  Kwa nini walimdharau Yesu???

  Walimuona kama mwenzao,wakauliza ,"je huyu si mwana wa Yosefu?"(Luka 4:22).Swali hilo limejaa na kusheheni dharau,kejeli,bezo,mapuuzo na manyanyaso.Pengine tunakosa neema kwa kukosa kutambua wajumbe wa Mungu.
  "Hakuweza fanya muujiza huko,isipokuwa kuponya wagonjwa wachache(Marko 6:5).Kuishi kwa Yesu muda mrefu Nazareti kulimfanya aonekane wa kawida.Nazareti walikosa neema ambazo ziliwaendea watu wengine.Bwana huwadharau wenye wivu na hatoi miujiza kwao.

  2. Mazoea yana tabu,Mazoea huleta dharau.

  Kijana anaweza akawa anamsalimia mtu mkubwa "shikamoo".Lakini akimzoea sana anamsalimia "Habari za leo".Baadhi ya watu hudahrau wengine kwa vile wanakaa sehemu fulani.Katika miji mikubwa huwa kuna matabaka,matabaka ya juu,ya kati na ya chini.Ukimwabia mtu nakaa sehemu fulanikama ni maskini anaweza kukudharau.
  Watu wakikudharau jua wewe sio wa kwanza kudharauliwa.Walimdharau mpka Yesu,iweje wewe??

  Wengine wakikukataa Mungu hajakukataa.

  3. Mazoea huzaa kutothamini.

  Bidhaa ikionekana sana kwenye soko bei yake hupunguakwa kiasi kikubwa,nakubaliana na Charles De Gaulle mwandishi wa kifaransa (1890-1970) aliyesema "Hapawezi kuwepo hadhi kubwa bila kuwepo fumbo au usiriusiri kwa vile mazoea huleta dharau".

  Mfalme Daudi alidhamini kazi yake kama mfalme,akizingatiaa itifaki lakini kadiri muda ulivyozidi kwenda mazoea huzaa kutothamini.Itifaki zote aliziweka kando na kumchukua mke wa mfanyakazi wake.

  4. Mazoea huondoa hofu.

  Kadiri ya La Fontaine (1621-1695) "Mtu wa kwanza kuona ngamia alikimbia; wa pili alithubutu kumtazama toka mbali; wa tatu alimfunga hatamu kuzunguka kichwa chake."

  Mazoea huondoa hofu.Socrates mwanafalsafa wa kigiriki alikuwa na mwanafunzi aliowafundisha.Alikuja kugundua kuwa walizoea kwenda kwenye nyumba za malaya.Siku moja wakati akipita mitaani karibu na nyumba hizo,Mwanafunzi wake mmoja alipomuona akarudi ndani ya nyumba.Socrate alimfuata huko na kumwambia."Usiogope kutoka,Ogopa kuingia".

  Huu ni ujumbe mzito kwa mtu ameingia pabaya.Usiogope kuacha dhambi.Ogopa kutenda dhambi.

  Ili kuyatokomezea mbali mazoea tunahitaji sauti ya kinabii.Huko niwani watu walikuwa wana mazoea yao mpaka hapo ilipotokea sauti ya kinabii ya Yona.Kuacha mazoea kunahitaji mtu ashtuke kuacha mazoea kunahitaji utafiti.

  Tunasoma hivi katika Biblia:"Naye Nathaeli akamwuliza Filipo"Je kitu chema kutoka Nazareti?"Filipo akamwambia,"Njoo uone" (Yohane 1:46)


  By Richard Edward

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.