Sunday, May 1, 2016

MCHUNGAJI: RAIS JPM AANDALIWE MKESHA WA MAOMBI.

Chief Hope | 4:30:00 AM |
Mchungaji wa Kanisa la AGCT, Mbagala, Samuel Mihogu amewataka watumishi wengine wa Mungu nchini hususan wa jijini Dar kufanya mpango kwa kuchagua siku moja ili kukesha kwa maombi ya kumlilia Mungu azidi kumlinda Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’

Soma: Askofu Gwajima Asema Haya Kwa Mh. Magufuli Na Mafisadi.

Akizungumza wiki iliyopita jijini Dar, Mchungaji Mihogu alisema kuwa, kwa mwendo wa Magufuli kikazi anaamini atazalisha maadui, hivyo watumishi wa Mungu wanatakiwa kumwomba Mungu ashushe ulinzi wake juu ya rais ili wabaya wake washindwe kwa kuanzia

“Magufuli anafanya kazi kubwa sana na nzito. Kutetea kwake wanyonge kwa kuwatumbua vigogo wanaokula pesa za umma lazima kuna watu hawatapenda, kwa hiyo mimi nawaomba wachungaji wengine tupange namna ya kutafuta siku moja tu ya kukesha Uwanja wa Taifa au Leaders (Dar) kwa maombi ili kumlilia Mungu amshushie ulinzi. “Najua serikali inampa ulinzi wa kutosha lakini maandiko yanasema mlinzi wa kweli ni Mungu. Kwa hiyo pamoja na ulinzi wa serikali, lakini Mungu lazima ahusike,” alisema mchungaji huyo. 

Akaendelea: “Kuhusu kulindwa hata Magufuli mwenyewe analijua ndiyo maana katika hotuba zake zote anawaomba Watanzania wamwombee kwa vile kazi anayoifanya ni ngumu"

Source: Rumaafrica blog & Ijumaa Wikienda

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

0 comments:

 
Content By Chief Hope | Facebook | Twitter | Copyright ©2016 TIM HEAVEN