Monday, April 18, 2016

MADHARA YA KUVUTA SIGARA.

Chief Hope | 8:27:00 AM |
Ufutaji sigara huathiri mwili kwa njia tofauti na madhara yake ni makubwa kiafya. Inakadiriwa kuwa, hadi sasa kumegunduliwa kemikali zipatazo 7,000 katika moshi wa sigara ambapo 250 kati ya hizo ni sumu na 70 zinasababisha kansa

Mvutaji mdogo hutumia nusu ya pakiti ya sigara kwa siku na kujikuta akiathiri mwili wake kwa kemikali hizi mara 3500 kwa mwaka. Mada na kemikali zilizo kwenye sigara huathiri karibu kila kiungo mwilini kuanzia seli hadi mfumo wa kulinda mwili.

Kemikali zilizoko kwenye moshi wa sigara huingia katika mapafu na kuenea katika mwili mzima na kusababisha madhara makubwa kwa njia mbalimbali

Soma: Madhara ya kutoa mimba

Ingawa mada hizo haribifu zilizoko kwenye moshi wa sigara ni nyingi, lakini tatu ni hatari zaidi zikilinganishwa na nyingine. 

Mada hizo ni nikotini, carbon monoxide na tar

Nicotine huufikia ubongo sekunde 7 hadi 10 baada ya moshi wa sigara kuvutwa na kemikali hiyo hutapakaa katika sehemu nyingi za mwili hata katika maziwa ya mama. 

Nikotini ni kemikali sumu ambayo kwa muda mrefu sana inatumiwa kama dawa ya kuuwa wadudu na sumu ya panya. Inachukua nafasi ya pili kama sumu kali kabisa kutokana na athari yake mbaya kwa mwili wa binadamu.

Tar ni kemikali inayosababisha kansa mwilini inayopatikana katika tumbaku ambayo huharibu jeni muhimu zinazozuia ukuaji holela wa seli ili zisiwe za saratani

Carbon monoxide ni gesi yenye madhara inayopatikana katika moshi wa sigara ambayo hujishikiza katika hemoglobin kwenye seli nyekundu za damu na kuzizuia zisiweze kubeba vyema oksijeni kama inavyotakiwa. 

Suala hilo husababisha mtu apatwe na dalili za kuwa na sumu ya gesi hiyo mwilini. Tunapaswa kujua kuwa, kuvuta sigara huwasababishia maradhi mbalimbali wenye kuvuta sigara kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na wasiuovuta. 

Soma: Madhara Ya Makeups

Miongoni mwa maradhi hayo ni magonjwa ya moyo, kiharusi, kansa ya mapafu, matatizo katika mfumo wa kupumua yanayojulikana kama COPD na mengineyo.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

0 comments:

 
Content By Chief Hope | Facebook | Twitter | Copyright ©2016 TIM HEAVEN