Wednesday, April 6, 2016

UNAJUA KWAMBA SMARTPHONE YAKO INAWEZA KUATHIRI AFYA YAKO?

Chief Hope | 1:12:00 PM | |
Matumizi ya simu za kisasa (smartphones) kwa muda mrefu huleta athiri kwenye mwili (afya) yako.

Hatuwezi kufikiria kuwa tunasababisha madhara makubwa kwa kutumia muda mrefu kwenye simu zetu za kisasa (smartphone au tablet), hasa kwa vijana waliochini ya umri wa miaka 24 ambao hawawezi kugeuza macho yao mbali na simu zao hata kwa sekunde moja.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na kituo cha Afya cha Uingereza cha Simpyhealth kimedhihirisha kuwa asilimia 84 ya watu waliofanyiwa utafiti wenye umri kati ya miaka 18 na 24 walikuwa wakisumbuliwa na maumivu ya mgongo yanasobabishwa na matumizi ya simu, kompyuta na vifaa vingine vya umeme kwa muda mrefu hasa wanapolala.

Soma: Madhara ya kutazama picha na video za uchi.

Utafiti huo umeonyesha kuwa matumizi hayo ya muda mrefu husababisha matatizo ya kiafya, kama maumivu ya shingo (hasa kwa kuangalia simu au kucheza michezo ya kompyuta kwa muda mrefu). Pia husababisha maumivu ya kwenye mabega, mshtuko wa mishipa, na hata badae kusababisha maumivu ya uti wa mgongo.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

0 comments:

 
Content By Chief Hope | Facebook | Twitter | Copyright ©2016 TIM HEAVEN