Sunday, May 1, 2016

UMIHIMU WA MATUMIZI ZA TANGAWIZI KWA AFYA

Richard Edward | 4:44:00 PM |

IMPORTANCE OF GINGER/UMUHIMU WA TANGAWIZI KWA AFYA
Katika miaka 500 iliyopita tangawizi ilianza kutumika mashariki ya mbali, kama vile China na India wakitumia kwa kutibu maradhi mbali mbali.
 

Katika hili zao la tangawizi kuna vyanzo vya:
Mangenisium
Mangnese
Potasium
Copper
Vitamini B6

Tangawizi ina umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu. Sana sana tangawizi hutumika kama kiungo katika mapishi. Manufaa yake kiafya ni kama ifuatavyo.

Soma: Maji Ya Vuguvugu Tiba Ya Magonjwa Yafuatayo

Tumbo:

Tangawizi inatumika kutuliza maumivu ya tumbo, yanayotokana na matatizo ya usagaji chakula, kuharisha, kuvimbiwa, n.k. Inapotumiwa katika chakula tangawizi husaidia usagaji chakula. Aidha tangawizi humuongezea mtu hamu ya kula.
Kichefuchefu na Kutapika:
Utafiti unaonyesha kuwa tangawizi ni tiba mufti kwa matatizo haya. Aidha huweza kutumiwa kupunguza tapishi inayotokana na uja uzito.
Matatizo ya Moyo: 

Tangawizi huimarisha moyo wa binadamu na kumwepushia maradhi ya moyo. Hii ni kwa kuwa inapunguza kiwango cha mafuta mwilini.
Matatizo ya Kupumua:

Huondoa homa ya mafua, hutumika kutibu pumu, na pia kufungua mfumo wa upumuaji hasa inapotumika pamoja na asali.
Maumivu:
 
Huondoa maumivu ya misuli, kichwa, na shinikizo la mawazo, kisunzi, na kukosa umakini.
Malaria

Husaidi kutibu Malaria na Homa ya Manjano.
Figo:
Inaaminika kuwa tangawizi inatibu tatizo la vijiwe vya kwenye figo.
Nywele:
Aidha hutumiwa kutunza nywele, kwa kuwa huondoa uyabisi (Dandruff.)

Soma: Madhara Ya Kuvuta Sigara.

Saratani: 

Hutumiwa na wataalamu wa kimatibabu katika tiba ya saratani.


By Richard Edward

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

0 comments:

 
Content By Chief Hope | Facebook | Twitter | Copyright ©2016 TIM HEAVEN