Monday, May 2, 2016

SIFA 7 ZA MWANAMKE WA KUOA (WIFE MATERIAL).

Chief Hope | 9:18:00 AM |
Wapo wanawake ambao wao wanajua kila siku ni Ijumaa, yaani hawatambui kwamba kuna Jumamosi na Jumapili pia. Watu hawa ni wale wanaodhani maisha ni raha tupu na kwamba wanaoishi kwenye shida ni wajinga. Ukweli hauko hivyo, maisha yana changamoto nyingi sana. Kuna siku mambo yanaweza kuwa si mazuri lakini siku nyingine mambo yakawa supa. Mwanamke wa kuoa lazima ajue hivyo.

1.HANA TAMAA ZA PESA 
Katika maisha ya sasa mwanamke anayependa sana pesa ukikubali awe mkeo mtasumbuana sana. Kwa maana hiyo mwanamke ambaye utagundua hana tamaa ya pesa, kwamba ikiwepo, ikikosekana anabaki kuwa yeye, huyu ni ‘wife material’. 

2.HAYUKO TAYARI KUKUONA HUNA AMANI 
Mwanamke ambaye unaona kabisa unapokuwa na matatizo anaumia, anahaha kuhakikisha anakurudisha kwenye hali ya kawaida, huyo anafaa kuwa mkeo.

Soma: Sifa 6 Za Mwanaume Anayestahili Kuwa Mumeo.

3.ANAPENDA WATOTO 
Utajuaje kama ana mapenzi na watoto? Iko hivi; katika uhusiano wenu ukiona ni mtu wa kupendapenda sana watoto wa marafiki zake, kuwanunulia zawadi, kuwashauri wenzake namna nzuri ya kuwalea watoto, hata akija kupata wa kwake itakuwa ni hivyohivyo. 

4.HESHIMA KWA KILA MTU 
Msichana ambaye anaheshimu kila mtu, mdogo na mkubwa, anawapenda na kuwaheshimu ndugu, jamaa na marafiki zako, huyu ana sifa ya kuwa mkeo pia. 

5.ANAJISHUSHA 
Ogopa sana mwanamke ambaye anataka usawa. Anayekufaa ni yule anayejua yeye ni mke, na wewe ni mume. Anayetambua kuwa, mwanaume ndiye kiongozi wa familia. 

6.ANAKUONGOZA KWENYE MEMA 
Kama mpenzi wako ni wa kukutaka kila siku muende baa au mfanye madili hatari ili mpate pesa, huyu hana sifa ya kuwa mkeo. Mke ni yule ambaye atakuongoza kwenye kutenda mema na kuacha mabaya. Kwa mfano kama unakunywa pombe atakushauri uache, kama siyo mtu wa ibada, atakushawishi umjue Mungu wako na mambo mengine kama hayo. 

7.ANAJUA MAISHA NA MAPENZI 
Mapenzi yanachukua sehemu kubwa ya maisha ya binadamu. Kwa maana hiyo mwanamke anayekufaa wewe ni yule ambaye anakupenda kwa dhati kabisa lakini pia anajua maisha

Soma: Sifa Tano Unazotakiwa Kujua Kabla Ya Kuoa/kuolewa

Endelea kusoma kila siku maishahalisi blog ili kupata vitu vizuri zaidi vya kuboresha maisha yako.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

0 comments:

 
Content By Chief Hope | Facebook | Twitter | Copyright ©2016 TIM HEAVEN