Friday, June 10, 2016

MISEMO 6 INAYOKWAMISHA NDOTO NA MAFANIKIO YAKO.

Chief Hope | 3:04:00 PM |
Kumekuwa na misemo mingi mitaani ambayo kwa namna moja au 
nyingine inaathiri au inaua kabisa ndoto za watu wengi. Watu wamekuwa wakiiga vitu katika jamii bila hata kuuliza kwa nini mtu huyu anafanya hivi. 

Soma Hapa: Siri Za Matajiri Wakubwa Zafichuka.

Kuiga mitindo ya kimaisha nalo limekuwa ni jambo ambalo linawaathiri watu wengi sana. Kuishi nje ya malengo uliyojiwekea na kukata tamaa ya maisha limekuwa tatizo sana. Kuishi maisha ambayo hayana furaha, upendo, amani ni tatizo miongoni mwa 
watu wengi.

1. Kila Kukicha Afadhali Ya Jana.
2. Bado Nipo Nipo Kwanza.
3. Fedha Ni Shetani
4. Tumia Pesa Ikuzoee/Ukipata Tumia Ukikosa Jutia.
5. Aliyekupa Wewe Ndiye Aliyeninyima Mimi.
6. Sina bahati. 

Kwa hiyo, watu wanatakiwa kuacha kuzitumia kauli hizi na 
kubadili mtazamo wa fikra, mambo ya kuamini mafanikio ni kwa watu waliosoma tu, au watu wa ukoo Fulani au kabila Fulani ndio wana haki ya kufanikiwa siyo kweli. 

Hakuna mafanikio ya haraka, usidharau biashara ndogo na usijidharau wewe mwenyewe bali jiamini katika kuwa mshindi na siyo mshindwa.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

0 comments:

 
Content By Chief Hope | Facebook | Twitter | Copyright ©2016 TIM HEAVEN