Wednesday, July 27, 2016

FAHAMU ATHARI HIZI ZA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA MAHUSIANO.

Chief Hope | 11:57:00 AM |
Athari za Uhuru wa kujieleza ndani ya WhatsApp, Facebook , Instagram
Hata hivyo hapo katika kujielezea ndipo kunapoweza leta matatizo badala ya kumsaidia mtumiaji wa mtandao. Nazungumzia pale ambapo mtu badala ya kukaa chini na mhusika na kumueleza malalamiko yako, wewe unatoka na kuenda kutangaza matatizo yako au kutoridhika kwako au hasira zako huko mtandaoni.

Status/Posts za WhatsApp, Facebook, Instagram zinasema mengi

Kuna watu unaweza jua mood zao kupitia status wanazoweka. Kwa yule ambayo amekukosea au mliye katika mfarakano, yeye hatojisikia vizuri hata kidogo, na huko unapoenda kutangaza wala hakuna wa kukusaidia.

Soma: Wanawake Shtukeni! Sera Za Haki Sawa Chanzo Cha Kuvuruga Ndoa Zenu.


Tafsiri ya posts zako za WhatsApp, Facebook, Instagram

Jambo lingine la kukumbuka ni kuwa kama unapopost malalamiko, kashfa au kejeli kwa kuwa umekasirishwa au unahisi kuonewa na mtu fulani, unajijengea picha mbaya kwa baadhi ya watu kuwa wewe si mzuri katika mahusiano ya mtu na mtu, hivyo watu wakae mbali nawe, kwani hujui namna ya kumaliza matatizo kati yako na watu unaohusiana nao, badala yake unakimbilia mtandaoni.

Athari zake

Unapojionyesha kuwa hauna uwezo wa kumaliza matatizo yako bila kuenda mtandaoni, unajiweka katika mazingira magumu mfano ya kupata kazi, au kupata washirika wa kufanya nao dili za biashara n.k kwakuwa wataogopa kuaibishwa mtandaoni.

Pia kujizoesha kukimbilia mtandaoni kutangaza matatizo yako badala ya kutafuta njia ya kuyamaliza huko pembeni, kunadhoofisha uwezo wako wa kujenga mahusiano bora.


Hitimisho

Pamoja na umuhimu wa mitandao ya jamii ya kutuweka karibu na watu wengi, tusisahau kujenga mahusiano ya mtu mmoja mmoja. Na lolote linalotokea baina yako na mtu au kundi fulani huko nje ya mitandao ya kijamii, jitahidi ulimalize huko huko nje, na sio kulipeleka mtandaoni kana kwamba huko mtandaoni kuna majaji wa kukupatia haki.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

0 comments:

 
Content By Chief Hope | Facebook | Twitter | Copyright ©2016 TIM HEAVEN