• Isikupite Hii

  SOMA MAKALA, HABARI MBALI MBALI NA MUZIKI WA INJILI TZ

  August 1, 2016

  TABIA 9 ZA KIONGOZI DIKTETA.

  Mara nyingi tunapozungumzia kiongozi au viongozi watu hutilia mkazo kwa Rais, Viongozi wa vyama, wabunge, Mawaziri, Wakuu wa mikoa, Madiwana n.k tu, La! Hasha kiongozi anaweza kuwa boss wako kazini au ofisini, Mme, Baba au mama nyumbani, au viongozi wa dini pia.

  Hizi baadhi ya tabia za kiongozi dikteta.
  1. Hakuna kuuliza maswali.
  2. Hakuna makosa. 
  Kiongozi huyo hafanyi makosa, yote anayoyasema au kuyatenda yako sawa kabisa. 
  3. Sheria inakuwa upande wake ama kundi lake na anawataka watu wafanye vitu bila kuliza maswali china ya mamlaka yake.
  4. Anawataka watu wafanye mambo kwa ubora nyakati zote. Hakuna kukosea, ukikosea kidogo tu hauna kazi tena.
  5. Hakuna uhuru wa watu kusema wala kukosoa.

  Soma: Nchi 10 Zenye Watu Wenye Iq Ndogo Zaidi Duniani. (Wastani)

  6. Mara zote kiongozi dikteta huubiri ubaguzi. Yeye au wao ni bora kuliko wengine wote duniani.
  7. Hupenda vita. Anasikia raha akiwa anapambana na watu wengine au mataifa mengine.
  8. Dikteta anajua kuna nguvu katika maarifa ndio maana atafanya juhudi zote kuhakikisha watu anaowangoza wanakosa maarifa.  
  9. Chama kimoja, 
  Kama ni taifa linakuwa na mfumo wa chama kimoja tu, hakuna mfumo wa vyama vingi.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

  Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk