• Isikupite Hii

  SOMA MAKALA, HABARI MBALI MBALI NA MUZIKI WA INJILI TZ

  August 5, 2016

  HASARA 13 ZA KUJIPENDEKEZA.

  1. Hauwezi kumkemea huyo unayejipendekeza kwake hata kama anakosea. 
  2. Unakuwa Mtumwa kwa huyo unayejipendekeza kwake. 
  3. Unaifanya akili yako ishindwe kuzalisha  matunda maana Unakuwa Tegemezi kwa huyo unayejipendekeza kwake. 
  4. Utajikuta unakosana NA watu hasa wakimkosoa huyo unayejipendekeza kwake. Maana huntokubali akosolewe mbele yako. 
  5.Inakufanya kuwa mnafiki  ,Maana hata wewe kwenye uvungu wa moyo wako kuna vitu unaviona havipo sawa lakini  "UNAMEZEA TU " Kulinda kufukuzwa. 
  6. Inakuharibu kisaikolojia ,hasa pale ambapo  Hautapata kile Ulichokitegemea kwa Huyo unayejipendekeza kwake. 

  Soma: Madhara Ya Kufanya Tendo La Ndoa Kabla Ya Ndoa.

  7.Inakufanya Uyanyonge MAONO uliyonayo kwa mikono yako mwenyewe, maana Muda mwingi unatafuta Jinsi ya kumpendeza  Huyo unayejipendekeza kwake. Badala ya kuwekeza Muda wako kwenye MAONO  Binafsi.
  8.Kunakufanya Huyo  Unayejipendekeza kwake  awe  "MUNGU MTU " ,Hivyo unajikuta unamsujudia kwa kila jambo.
  9. Hauwezi kufanya MAAMUZI Binafsi  ni hadi huyo unayejipendekeza kwake akuamilulie, akikataa ndiyo basi tena. 
  10.Utagombana NA watu mara kwa mara, maana kila atakayejionyesha kuwa karibu  NA  huyo unayejipendekeza kwake, Utampiga mawe maana unafikiri, anaichukua nafasi yako. 
  11. Inakufanya uthamani wako Ushuke kabisa NA kudharaulika , Maana unaishi kwa kumtegemea Mwanadamu mwenzako bila yeye haukai mjini. 
  12. mungu wako anakuwa ni huyo UNAYEJIPENDEKEZA KWAKE. 
  13.Hauwi Mwanaume halisi /Mwanamke halisi, Maana walio Halisi wanayo misimamao Binafsi.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

  Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.