• Isikupite Hii

  SOMA MAKALA, HABARI MBALI MBALI NA MUZIKI WA INJILI TZ

  August 15, 2016

  Picha za ngono zinavyo-athiri afya za vijana Duniani.

  Daktari mmoja wa tiba ya maungo amesema kuwa vijana wadogo wanahatarisha afya yao ya uzazi kwa kuangalia sana picha za ngono katika mitandao ya kijami.

  Angela Gregory kutoka hospitali ya chuo kikuu cha Nottingham amesema kuwa idadi kubwa ya vijana walio kati ya umri wa miaka 18 hadi 24 wanatafuta usaidizi kutokana na maswala tata ambayo hayajawahi kuonekana miongoni mwa wagonjwa walio na umri mdogo katika kipindi cha miaka 10.

  Soma: Madhara Ya Kutazama Picha Na Video Za Uchi.

  Awali watu wazima ndio waliokuwa wakitembelea vituo vya afya wakikabiliwa na matatizo kama kushindwa kusimamisha uume kutokana na magonjwa kama vile sukari ama yale ya moyo.

  Lakini utazamaji wa picha za ngono mitandaoni unaharibu mahusiano ya ndoa kwa kuwa vijana wengi wanavutiwa zaidi na picha za ngono katika mitandao badala ya binaadamu.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

  Kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.