Wednesday, October 19, 2016

MAMBO NANE (8) MAKUBWA YANAYOWASUMBUA WATU WENGI DUNIANI

Richard Edward | 3:27:00 PM |

 MAMBO NANE (8) MAKUBWA YANAYOWASUMBUA WATU WENGI DUNIANI

Mambo yanayoongoza kwa kuwachanganya watu kimaisha na wakati mwingine kuwafanya waione dunia ni chungu.

Nafanya hivi kwa sababu kuna mambo ambayo huwa tunayakosea bila kujua, tunafanya maamuzi ambayo yanakuja kutugharimu baadaye.

Isikupite Hii: Unawafurahisha Vipi Wazazi Kipindi Cha Uhai Wako!!

Yapo mengi lakini leo nimeona nikupe haya machache ambayo yanaweza kukusaidia katika maisha yako

Mume/mke asiye sahihi

Huwezi kuwa na maisha ya furaha kama uko na mke au mume asiyekujali, asiyekuonesha mapenzi ya dhati. Tukumbuke wapo watu ambao wana kila kitu lakini mapenzi yamekuwa yakiwachanganya sana kimaisha.

Ndiyo maana inashauriwa kuchagua mpenzi sahihi ambaye atakuwa ni mmoja wa watu wa kukufanya uwe na furaha maishani mwako na siyo wa kukufanya ujute kuzaliwa mwanadamu.

Madeni

Hakuna jambo linalowakosesha baadhi ya watu amani kama madeni. Wapo waliofikia hatua ya kujiua kwa sababu ya kudaiwa kila kona. Licha ya kwamba kila mmoja kuna wakati anakopa, hutakiwi kuiendekeza tabia hii na kama unaweza, epuka kukopa na utajiona ni mtu huru.

Kukosa chanzo cha kipato

Maisha ya sasa bila kufanya kazi huwezi kuwa na maisha mazuri kwani ndiyo inayoweza kukupatia kipato cha kuyaendesha maisha yako. Hata hivyo, ili kukufanya uweze kujikimu kimaisha, hakikisha unafanya kazi bila kuchagua kazi.

Isikupite Hii: Kutoka Kuajiriwa Mpaka Kujiajiri: Mambo 8 Muhimu Ya Kuzingatia

Epuka sana kukaa vijiweni huku ukitarajia fulani atakusaidia. Ukiwa mtu wa sampuli hiyo ipo siku utalia na kusaga meno kwani huwezi kusaidiwa kila siku.

Ugumu wa maisha

Binadamu yeyote lazima apate mahitaji muhimu kama vile chakula, mavazi, sehemu nzuri ya kulala na matibabu akiumwa. Endapo utajihakikishia yote hayo katika kiwango kinachostahili, maisha yako yatakuwa ya furaha

Kinyume chake utakuwa ni mtu wa kushika tama na usipojiangalia unaweza kutafuta kamba ya kujinyongea.

Kuishiwa

Fedha ndo’ ni nyenzo muhimu sana katika maisha ya binadamu, ukikosa fedha lazima kichwa kikuume. Wapo ambao wanakosa amani wanapofikiria matatizo yanayoweza kuwakumba huku wakiwa hawana pesa kabisa.

Ndiyo maana inashauriwa kwamba, unapopata fedha usitumie zote, weka akiba pale inapotokea umepata pesa ya ziada.

Hiyo itakufanya uwe na amani ukiamini kwamba, uko tayari kukabiliana na tatizo lolote mbele yako litakalohitaji fedha.

Kukosa upendo/Kuchukiwa

Hata uwe na mamilioni vipi, kama watu wanaokuzunguka hawakupendi, huwezi kuwa na furaha. Ndiyo maana unatakiwa kutumia gharama yoyote kujihakikisha upendo kutoka kwa ndugu zako, majirani, marafiki na watu ambao unakutana nao katika mihangaiko yako.

Isikupite Hii: Mambo Sita (6) Yatakoyo Kusaidia Kuanza Kujitegemea

Ukikosea kidogo, ukachukiwa na kila mtu ni lazima maisha utayaona machungu. Hutakuwa na mtu wa kucheka naye. Wengi waliokosa upendo kwenye jamii zao mwisho wao umekuwa mbaya.

Mkusanyiko wa matatizo

Hakuna binadamu asiyekumbwa na matatizo ambayo mara nyingi hufanya amani itoweke. Hata hivyo, inaelezwa kuwa, ili kuepuka msongo wa mawazo, hakikisha kila tatizo linalotokea mbele yako unalitatua haraka.

Endapo utakumbwa na tatizo dogo leo, ukaliacha hadi kesho na likatokea lingine, utakuwa umejikusanyia tatizo kubwa linaloweza kukusumbua. Unapopatwa na tatizo, omba msaada na ulitatue kwa wakati ili ubaki na amani.

Uzazi usio na mpango

Wapo watu ambao unaweza kupishana nao barabarani wakiongea peke yao. Hao ni wale ambao mambo yamewazidia. Yawezekana mtu akawa ameona fahari kuzaa, akazaa watoto wengi lakini linapokuja suala la kuwatuza, inakuwa ni pasua kichwa kwake/vigumu.

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kuimarisha Mfumo Bora Wa Uwekaji Wa Akiba

Unakuta huyu analilia nguo za shule, yule kafukuzwa ada, nyumbani hakuna chakula, mara mwingine anaumwa. Unadhani katika mazingira hayo halafu usiwe na kitu mfukoni hali itakuwaje?

By Richard Edward 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.

0 comments:

 
Content By Chief Hope | Facebook | Twitter | Copyright ©2016 TIM HEAVEN