• Isikupite Hii

  SOMA MAKALA, HABARI MBALI MBALI NA MUZIKI WA INJILI TZ

  October 10, 2016

  UNAZIFAHAMU FAIDA ZA KULA TUNDA LA TIKITI MAJI? ZIKO HAPA.

  Tikiti maji linatajwa kuwa na kiwango cha maji kwa asilimia 92 huku asilimia 8 zilizosalia zinatajwa kuwa na faida lukuki ambazo wengi hawazifahamu.

  Kama mlaji wa tunda la tikiti maji unapaswa kufahamu faida zipatikanazo katika tunda hili kwani lina vitamini nyingi, kwanza tikitimaji lina vitamin A ambayo huboresha afya ya macho na kuondoa sumu mwilini

  Isikupite Hii: Maradhi Haya Hutibiwa Na Ulaji Wa Mboga Ya Majani Mchicha.

  Tunda hili pia lina vitamin C ambayo husaidia kuboresha kinga ya mwili na kuponya majeraha, kuboresha afya ya meno na fidhi na vitamin B husaidia ubongo kufanya kazi na pia tunda la tikiti maji husaidia kubadilisha protini kuwa nishati.

  Pia tunda hili linatajwa kuwa na kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani na pia lina madini ya potassium ambayo ni muhumu kwa afya ya binadamu. 

  Tunda hili hufanya kazi ya kuupa uwezo mkubwa mfumo wa fahamu na kumwepusha mtu kupata shinikizo la damu, pia tunda hili lina ‘amino acid’ na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake lakini kubwa zaidi husifika kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.