• Isikupite Hii

  January 13, 2017

  Jinsi ya kutengeneza fedha kupitia kipaji (hobby) chako.

  Maisha yanapaswa kufurahiwa. Lakini kama hufurahii kazi yako, lazima ikuchoshe kufanya kazi mchana kutwa. Kila mtu lazima ana hobby anayoifurahia. Ni njia ya kujionesha mwenyewe na kujisikia vizuri. Kinachofurahisha zaidi ni kuwa wakati mwingine unaweza kuifanya hobby yako ikulipe.


  1. Kuuza bidhaa
  Unafurahia kutengeneza vitu? Viuze. Watu wengi tu wanauza bidhaa zao. Hakikisha una kitu maalum ambacho mwingine hana.

  2. Husisha wengine

  Baadhi ya hobby kama vile kucheza vvyombo vya muziki au ujuzi mwingine, ni nzuri kuwahusisha watu. Kumfundisha mtu kucheza chombo cha muziki au kutengeneza kitu kunaweza kulipa. Toa mafunzo mara kwa mara, kila wiki au kila mwezi au toa semina kwa watu wenye hobby kama yako lakini wanaopenda kujua zaidi.

  3. Tafuta kazi unayoendana nayo
  Baadhi ya hobby ni ngumu kuzigeuza kuwa biashara. Jaribu kuangalia kazi ambazo zinaendana na hobby yako. Unapenda maua? Kuwa mtu wa bustani. Unapenda kufanya mazoezi? Kuwa trainer. Unaweza usipate kile kile unachotaka, lakini ukipata kazi ambayo unaweza kushare maarifa kwenye suala Fulani ni kitu cha kizuri.

  4. Weka online
  Labda hupendi kuuza ama kufundisha. Blog kuhusu kitu hicho. Tengeneza website yako mwenyewe na share passion yako kwa wengine. Chukua picha na onesha ubunifu. Kadri watu watakavyoipata website yako, ndio utapata faida zaidi hasa kama unataka kupata matangazo. Ongea kuhusu mada kuvutia, share mambo yako, ni website yako kwahiyo fanya upendacho.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Kupitia FacebookTwitterInstagram ili kupata habari, makala juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.