• Isikupite Hii

  January 18, 2017

  Siri 7 zitakazomfanya umpendaye 'Mme' awe na furaha siku zote

  1. Baada ya kazi ngumu za wiki, mwandikie ujumbe mzuri sana wa kurudi nyumbani. Mtumie ujumbe wa upendo wa kumsihi aje nyumbani na pia wa kumkumbusha kuwa ni muda mwafaka wa kupumzika na wewe.

  2. Vaa nguo za chumbani huku ukimsubiri atoke kazini. Hii itamfanya kukupenda zaidi. Na kwa hakika atakubali jitahada zako na itamuongezea upendo kwako.

  3. Kama mwezi wako anarekebisha uso wake kama kunyoa ndevu, mfanyie hilo. Weka nyimbo za upendo kwa taratibu na kwa upole mnyoe. Wewe chukua muda wako na fanya hivi atajisikia kuwa anapendwa na anajaliwa.

  4. Chukua muda wako mkiangaliana machoni. Kubali na tambua uwepo wake, tambua marashi na manukato yake na joto lake. Na kama unajisikia hata kumbusu fanya hivo.

  5. Jifanye kumuhitaji. Mwanaume hutamani kuonekana kuwa yeye pekee ndiye anayekulinda, hivyo mwambie kuwa hujisikii vizuri na huwa unakuwa mpweke pale anapokosekana ama unajisikia vizuri na kuwa na amani pale anapokuwepo.

  6. Mkumbatie kwa ghafla. Onyo-fanya hivi pale ambapo mpo wawili tu ili kwamba asije akajisikia kuwa hayuko huru au amelazimishwa. Napendekeza fanya hivyo kwa muda wa dakika 5-6 afu mpe nafasi.

  7. Mnunulie tiketi ya mpira wa miguu au mpira wa kikapu ule ambao yeye angependa kuuona. Ili kuonyesha upendo nenda nae mkashabikie timu yake kwa pamoja.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

  Kupitia FacebookTwitterInstagram ili kupata habari, makala juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.