• Isikupite Hii

  SOMA MAKALA, HABARI MBALI MBALI NA MUZIKI WA INJILI TZ

  January 12, 2017

  Jinsi ya kutunza ndoa yako, hata kama kuna udanganyifu na usaliti.

  Hakuna siri kuoa ni kazi. Wachumba lazima wajifunze namna ya kutafuta suluhu na kubembeleza mahusiano pale matatizo yanapotokea. Kama mwanya wa uaminifu ukitokea kwa mke wako kwaajili ya udanganyifu alioufanya, usaliti huu unaweza kupelekea kukosa matumaini, huzua hasira na huondoa uaminifu kabisa kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke. 

  Watu wanaotarajia kuanza uhusiano wa kiuchumba ni vyema kutafuta washauri ili kuwashauri juu vitu vitakavyotokea vitakavyo sababisha ukosefu wa uaminifu na pia mambo yatakayo pelekea kuondoa matumaini lakini pia kuwashauri namna ya kutatua migogoro itayotokea ili kuwarudisha katika mahusiano mazuri yatakayowafanya kuwa pamoja, inaweza ikasaidia. 

  1. Imarisha mawasiliano.
  Ingawa inaweza kuumiza na kuumiza hakujabadili udanganyifu au ukosefu wa uaminifu uliotendeka, ndoa inatakiwa kujengewa kwa msingi wa ukweli na uwazi. Kuimarisha mawasiliano juu ya jambo lilitokea ambalo likapelekea udanganyifu, na inaweza kuwa ngumu sana kulijadili hili jambo kwa undani, lakini kwasababu ya kuweka amani ya moyo ni vizuri. Kama mke anaendelea kutunza siri hii italeta tatizo kubwa badala yake anatakiwa kuomba radhi na kuthamini hisia za mume wake ili kuweka ndoa yake katika hali nzuri.

  2. Anzisha mahusiano upya.
  Baada ya udanganyifu, ni vigumu sana kurudisha uhusiano kama ulivyokuwa mwanzo. Katika kurudisha uamuzi wenu dhabiti, muanze uhusiano upya. Mwanamke anaweza kumshtukiza mume wake na vitu vipya vitakavyoimarisha kama kumjali, upendo ulioboreshwa yaani zaidi ya mwazo, hata kumkumbatia kumbatia wakati wakiwa wote. Pale mwanamke anapomdanganya mwanaume, mwanaume hujisikia kuwa kutotakiwa katika jamii aliyopo na pia kutokuwa na mvuto. Kuwa nae karibu na kuonyesha jinsi uliyoathirika katika jambo hilo kunamuinua na kumuongezea ujasiri na kujiamini pia.

  3. Tafuta washauri wa ndoa.
  Kufanya kazi na hisia za ndani za mtu aliyedanganywa na mke inahitaji mtu aliyebobea katika ushauri kuhusu maswala ya mahusiano. Mshauri wa ndoa au wa familia yeye atawasaidia wote katika kutatua migogoro na kutokuelewana kwenu, na pia hata tabia mbaya za uvunjifu wa ndoa yenu na kuwapa njia bora zitakazofanya uhusiano wenu au ndoa yenu kuuendelea, na itawasaidia kuwa na mtu wa tatu ambaye atawasikiliza na kuwapa majibu yatakayoisaidia ndoa yako.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

  Kupitia FacebookTwitterInstagram ili kupata habari, makala juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.