• Isikupite Hii

  June 20, 2017

  Sifa tano unazotakiwa kujua kabla ya kuoa/kuolewa.

   SIFA TANO UNAZOTAKIWA KUJUA KABLA YA KUOA/KUOLEWA
  Kuna watu wenye tabia mbaya kiasi kwamba wapenzi wao wanajuta kuoana nao, wanaona ni heri zaidi kama wangeishi peke yao. Sasa, utamjuaje mwanaume aumwanamke mwenye tabia mbaya, ili ujiokoe na ndoa yenye utata?

  Isikupite hii: Je unaijua saikolijia ya mwenzi wako katika mahusiano!!

  1. Tabia zake haziendani na wewe.

  Kama tabia zako haziendani na mwanaume au mwanamke unayetaka kuoana naye, ujue mapema ya kuwa ndoa yenu itajaa mfurulizo wa matatizo bila kukoma na hivyo mtadumu katika migogoro na ugomvi usioisha.

  2. Huishusha hadhi yako mbele ya familia na rafiki zake.

  Atakuwa mume au mke mbaya kama umegundua tabia yake ya kupenda kuishusha hadhi yako mbele ya familia au rafiki zake. Hasa kama ni mwepesi wa mapungufu yako mbele ya rafiki zake, hata kabla hajakwambia lolote juu ya udhaifu wako, unamkuta mtu mzima anadiriki hata kuwaeleza rafiki zake juu ya udhaifu wako faragha, ukimjua huyo usithubutu ndoa.Ana sifa hizi 5? Usikubali ndoa

  3. Hawakubali wana familia na rafiki zako.

  Kama anakuwa mtu wa kusimamisha bendera nyekundu (red flag), kila mara unapojumuika na familia au rafiki zako, unatakiwa kuwamakini, anaweza kuwa mpenzi mbaya huyo!.

  4. Hapendwi na familia na hata rafiki zako pia.

  Kama sehemu kubwa ya rafiki na familia yako wanakushuhudia mambo mengi mabaya juu yake, ni vyema ukawa makini  na kuchukua tahadhari kwani yawezekana umepofushwa tu na hisia zako za mahaba juu yake, hivyo unashindwa kuyaona mambo mabaya yanayotazamwa na wengine. Familia na rafiki zako wanakupenda na wanataka uwe na maisha bora, kuwa makini.

  5. Kama hakuna muunganiko wa ndani ya moyo unaojisikia kati yenu.

  Mapenzi hutawaliwa na hisia kwa asilimia kubwa, usikubali kuwa na mtu eti kwasababu ni kijana mtanashati au ana urithi wa mali nyingi, Amini nakwambia penzi lenu halitodumu kabisa, yawezekana akaanza yeye au wewe kumsariti mwingine kwa kuuelekezea moyo wako kule unakojisikia upendo zaidi.

  Isikupite hii: Umuhimu wa kuandika husia wa mwisho.

  Ni heri ukosee njia au ukapoteza mali zako zote kwa kuwa unao uwezo wa kujipanga upya na ukajiimarisha tena, kuliko kukosea kuchagua mtu wa kuoana naye, kumbuka hilo ni janga lako la maisha.