• Isikupite Hii

  July 12, 2017

  Unamtambuaje rafiki mwenye dalili za kuja kuwa adui.

  Rafiki anaweza kuja kuwa adui au msaliti kwenye mambo mengi yakiwemo
  • Kwenye mapenzi
  • Kwenye biashara
  • Kwenye kupata nafasi kazini
  • Kwenye mahusiano na marafiki zenu
  • Kwenye mikataba au tenda

  Soma: Sababu 5 Za Mikwaruzo Katika Maisha.

  Dalili/Mazingira
  • Unasikia au unagundua anakusema vibaya kwa wengine, tofauti na akiwa na wewe
  • Unahisi au unagundua anakupinga au kukuonea wivu kwenye mambo fulani
  • Unahisi au kugundua nia yake ya kutamani kupata zaidi yako
  • Unahisi au kugundua kuwa ushauri anaokupa sio wa kukusaidia bali wa kukukwamisha huko mbeleni
  Unafanyaje?
  • Usimwamini sana mtu wa namna hii
  • Usijiachilie na kuwa wazi sana kwa mtu huyu
  • Pima ushauri wake na ikiwezekana uliza mtu mwingine pia.