• Isikupite Hii

  July 26, 2017

  TCU yatoa vyuo na programu zilizozuiliwa kufanya udahili kwa mwaka 2017/2018

  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kuuarifu umma kuwa, mwezi Septemba na Oktoba mwaka 2016 ilifanya uhakiki wa vyuo vyote vya elimu ya juu nchini ili kuhakiki ubora wa elimu inayotolewa vyuoni. Ripoti ya uhakiki ilionesha mapungufu kadhaa katika baadhi vyuo. 

  Kwa sababu hiyo, Tume imesitisha udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18 kwa vyuo vifuatavyo: 
  1. Eckenforde Tanga University 
  2. Jomo Kenyatta University, 
  3. Arusha Kenyatta University, 
  4. Arusha United African University of Tanzania 
  5. International Medical and Technological University (IMTU) 
  6. University of Bagamoyo 
  7. Francis University College of Health and Allied Sciences 
  8. Archibishop James University College 
  9. Archibishop Mihayo University College 
  10. Cardinal Rugambwa Memorial University College 
  11. Kampala International University Dsm College 
  12. Marian University College 
  13. Johns University of Tanzania Msalato Centre 
  14. Johns University of Tanzania, Marks Centre 
  15. Joseph University College of Engineering and Technology 
  16. Teofilo Kisanji University 
  17. Teofilo Kisanji University Tabora Centre 
  18. Tumaini University, Mbeya Centre 
  19. Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMCo) 2

  Aidha, kutokana na mapungufu katika vyuo mbalimbali imeamriwa kwamba jumla ya programu 75 kutoka vyuo 22 nchini zimesitishwa kudahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18. Kuona Programu ambazo zimesitishwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/18 tafadhali bonyeza hapa.