• Isikupite Hii

  November 13, 2017

  Nguvu ya maamuzi Part 11,nini kifanyike baada ya kufanya maamuzi mabaya
  “Maamuzi mabaya  uliyoyafanya nyakati za nyuma yanaweza yakawa ni sababu yaw ewe kuwa hivi ulivyo leo  lakini usiruhusu  yafanyike  kisingizio  cha wewe  kubaki  katika hali uliyonayo  maamuzi mazuri  ya sasa  yatafanya  mabadiliko  ya maamuzi  uliyoyafanya hapo awali” Joyce mayer
  Hakuna mwanadamu aliyekamilika wote hukosea Kuna msemo wa Kiswahili unasema ukimuona nyani mzee basi ujue amekwepa mishale mengi, tunayoyapitia yanatufundisha yanatuimarisha yanatufanya tuwe bora zaidi 
  1.       Kataa  kujisikia uchungu   ama kujutia  kwa maamuzi  mabaya uliyoyafanya;  Inatakiwa ujue kuwa   bado uko kwenye nafasi nzuri ya kukuwezesha kufanya maamuzi mazuri yatakayobadilisha hatima ya maisha, kujisikia uchungu unaporuhusu uchungu na majuto unaruhusu hali ya kujiona hauna thamani, ujasiri unaondoka hofu inatawala ndipo unaona kana kwamba hufai tena. kumbuka kuwa maamuzi mabaya hayaondoi thamani yako  kinachoondoa thamani yako ni vile unavyoyachukulia maamuzi uliyofanya  sasa nini kifanyike
  Badilisha mtazamo wako kuhusu makosa ya maamuzi yako  kwa namna ifuatayo
  ·         Kila mwanadamu  anakosea  na wewe umekosea kwa kuwa na wewe ni mwanadamu
  ·         Umekosea ili ujifunze kutokukosea hivyo kukosea si jambo baya kwa sababu ni darasa  ambalo mwalimu wake ni kosa lenyewe, ninapogundua nimekosea sitakiwi kujilaumu wala kujuta natakiwa nitafute Huyu mwalimu (kosa) amekuja kunifundisha somo gani tena natakiwa nijifunze kwa furaha  kwa sababu ninapofuzu kila darasa ninaenda hatua ya mbele zaidi
  ·         Umekosea ili uwe msada kwa  wengine ama uwanusuru wasikosee ama uwatie moyo  na kuwashauri watakapokosea
  ·         Umekosea kwenye jambo dogo kama tahadhari ya kukuepusha kukosea kwenye jambo kubwa
  Mtazamo wa aina hii utakusaidia kutochukuwa makosa  kama mzigo mzito wa uchungu na majuto  mtazamo huu hautakufanya uogope kukabiliana na matokeo ya maamuzi uliyoyafanya  mtazamo huu utakupa kumshukuru Mungu kwa kuruhusu jambo hilo Maana ni fursa ya wewe  kwenda hatua za mbele zaidi
  2.       Acha kujilaumu ama kulaumu  wengine
        watu wengi wanapogundua kuwa wamefanya maamuzi mabaya  hujilaumu,  kujilaumu hutokea pale nafsi yako inapokuhukumu kwa sababu ya maamuzi mabaya  na kulaumu wengine hutokea pale ambapo nafsi yako inakushuhudia kuwa watu au mtu Fulani ndiye aliyesababisha wewe kufanya maamuzi uliyoyafanya, badala  ya kujilaumu ama kulaumu wengine  chukua jukumu  la kukabiliana na madhara ya maamuzi uliyofanya  waswahili wanasema yaliyopita si ndwele tugange yajayo,  maandiko yana sema  yakale yamepita tazama yamekuwa mapya  usiruhusu  mawazo yanayokurudisha  kwenye mambo ya zamani yaliyokwisha kupita  wewe ni mtu mpya sasa, wewe ni shujaa sasa  wewe ni mtu mwema sasa unaweza sasa  Basi chukua  la  kubadilisha  maisha yako  kwa kufanya maamuzi mazuri sasa yatakayobadilisha maisha yako ya sasa na badaye

  3.       Makosa yakufunze kuwa bora zaidi ; Kufanya kosa si kosa ila kurudia kosa (msemo wa waswahili)  na pia kujua tatizo ni  nusu ya ufumbuzi wa tatizo   Makosa  yakufunze  kutokosa tena , maamuzi mabaya yakufunze  kufanya maamuzi  mazuri  , maandiko yanasema  angalia ni wapi ulipoangukia ukatubu , makosa ya awali yana nguvu kubwa ya kukufunza. Ili usirudie makosa ya nyuma ni lazima uwe tayari  kujifunza  kutokana  na makosa hayo, Makosa yasikuharibu Makosa yasikufanye ujilaumu  Makosa  ya nyuma yasikufanye ukate tamaa  Makosa yakufundishe kutorudia makosa tena  ili uwe bora zaidi

  4.       Jisamehe  wasamehe na wengine waliokukosesha kwa namna moja au nyingine; njia pekee ya kuondoa uchungu moyoni na kurejesha amani na furaha ya moyo ni kusamehe na kuachilia  kwa kufanya hivyo utakuwa umejiweka kwenye nafasi nzuri ya kutorudia makosa na kufanya maamuzi yenye tija kwenye maisha yako samehe ili na wewe usamehewe samehe kwani nao ni wanadamu samehe kwa kuwa wamekuwa sababu ya kukufanya uwe bora zaidi, samehe ili utue mzigo wa uchungu ndani ya moyo wako.

  5.       Usiangalie nyuma;Mara nyingi mtu anapogundua kwamba amefanya maamuzi mabaya huingiwa na hofu. Hofu inayoondoa ujasiri,  hali hii usababisha mtu huyu kujiona kana kwamba kila atakalofanya atakosea Makosa yapo ili kutuimarisha na kutufanya tuwe bora zaidi Hivyo si vema kutumia makosa ya nyuma kama rejea (reference)  ya maamuzi ya sasa  umegundua kuwa ulifanya maamuzi mabaya kubali kwamba  umekosea kubali kujifunza kutokana na hayo makosa  somo hilo likusaidie kuendelea mbele na kufanya maamuzi bora zaidi

  6.       usifiche makosa ;Kuna msemo wa Kiswahili unasema mficha uchi hazai  unapogundua umefanya maamuzi usifiche watu wengi wanapogundua wamekosea huficha makosa  kuficha makosa kunasababisha nafsi yako kuendelea kukuhukumu  na unakosa ujasiri wa kuendelea mbele sio lazima umtangazie kila mtu ajue kwamba ulikosea bali kuna watu wa karibu na wewe ambao huwa unawashirikisha mambo yako watu ambao wanaweza kukushauri unapokosea usifikiri wewe ndiwe wa kwanza kukosea  kunawaliokutangulia kukosea pia wapo waliofanya maamuzi hay ohayo uliyoyafanya  hawa ni watu ambao Mungu anaweza kuwatumia kukushauri nini cha kufanya kwa sababu walikwisha kupitia lile unalopitia endapo tu utakuwa tayari  kuwashirikisha   maandiko yanasema kwenye wingi wa mashauri hapaaribiki jambo

  7.       Tubu na Muombe Mungu wako ;Maandiko yanaema tukisema kuwa hatuna dhambi tunajidanganya bure, dhambi husababishwa na maamuzi mabaya tunayoyafanya;  hivyo tungeweza   kusema kwamba tukisema hatufanyi maamuzi mabaya tunajidanganya bure  lakini tukikubali na kutubu Mungu ni mwaminifu atatusamehe kabisa.  Usijihukumu kwa maamuzi yako Tubu na umuombe Mungu Unapotubu unairuhusu neema ya Mungu kukusaidia na kukutoa kwenye madhara ya maamuzi uliyoyafanya.

  UNAPOGUNDUA KUWA UMEFANYA MAAMUZI YASIYOSAHIHI  PATAMUDA WA KUTAFAKARI MAMBO YAFUATAYO ILI YAKUSAIDIE KUTOKURUDIA KUFANYA MAKOSA KWENYE MAAMUZI HAYO
  ·         ulifanya hayo maamuzi  ukiwa kwenye mazingira gani
   kunamazingira humpelekea mtu kufanya maamuzi yasiyo sahihi mfano mazingira ya ulevi huzuni, mihemko,ama furaha iliyozidi, msongo wa mawazo nk(rejea sura ya mazingira ya hatari kufanya maamuzi) unapopata muda wa kutafakari ni mazingira yapi yaliyokupelekea kufanya maamuzi hayo, hii itakusaidia kuwa makini na kuepuka kufanya maamuzi ukiwa kwenye mazingira ya namna hiyo.
  ·         nini kilikupelekea ufanye maamuzi hayo uliyoyafanya
  kila maamuzi yana ushawishi  uliopelekea maamuzi hayo   ushawishi huo ni kama tamaa, ushauri  kutoka kwa marafiki  wazazi n.k unapogundua ulifanya maamuzi mabaya ni vema pia ukatafakari  ni ushawishi gani ulikupelekea kufanya maamuzi hayo   hii itakusaidia kujiweka mbali na vitu vyenye ushawishi mbaya ili ili kujiweka kwenye mazingira salama ya maamuzi yako ya sasa nay a baadaye.
  MAMBO MUHIMU KUFAHAMU UNAPOGUNDUA UMEFANYA MAAMUZI MABAYA
  Ø  Neema ya mungu ipo kutusaidia wakati wa madhaifu; Madhaifu ya mwanadamu ni pamoja na kukosea  Mungu ameiachilia neema yake kupitia mwanae Yesu Kristo ili itusaidie  kutukomboa na madhara ya maamuzi mabaya tunayoyafanya  kwa neema yake tunasamehewa dhambi na kufutiwa makosa yetu Maandiko
  Ø  Mungu hutumia maamuzi mabaya uliyofanya kukupeleka hatua nyingine; Maamuzi mabaya humsababisha mtu aingie kwenye jaribu sasa maandiko yanasema Mungu huruhusu jaribu litupate ili atupeleke hatua nyingine maandiko yanasema heri yake yeye astahimilie majaribu maana yake; heri yake yeye ambaye anapokosea anakubali kuwa amekosea kisha anaanza kutafuta ufumbuzi wa makosa yake kwa imani ya ushindi, tena Mungu amesema anaporuhusu jaribu likupate basi huruhusu lile ambalo ni kipimo chako   tena amesema anaweka na mlango wa kutokea hivyo  unapojikuta umeingia kwenye jaribu kwa sababu ya  ya maamuzi uliyofanya usijihukumu kwa sababu ya maamuzi hayo Jua kwamba Mungu ameruhusu kwa ajili ya kukupeleka hatua nyingine 
  Ø  Mtu asikuhukumu kwa sababu ya maamuzi uliyoyafanya kwa sababu Mungu amekwisha kusamehe na neema yake ipo kukusaidia kushinda na kusonga mbele
  Ø  Kukosea kunakutengeneza ili uwe bora zaidi  Ili uweze kukabiliana na mambo makubwa zaidi
  Ø  Kukosea kufanya maamuzi hakukuondolei thamani yako
  Maamuzi juu ja maamuzi
  Unapogundua kuwa umekosea kwa kufanya maamuzi mabaya kuna maamuzi mengine utatakiwa uyafanye maamuzi haya ni kuamua sauti ya kuisikilizaili  kukabiliana na madhara ya maamuzi uliyofanya  Shetani atataka kuyatumia makosa yako kuendelea kukukandamiza  shetani ataendelea kukuonyesha ukubwa wa makosa yako tena  atazidi kukukumbusha,  shetani atafanya hivyo ili uzidi kuumia uzidi  kujilaumu na kujiona mkosa. Mungu atakusamehe na kufuta makosa ya maamuzi mabaya uliyofanya ,Mungu atakuambia sahau yaliyopita endelea mbele,  Mungu atakuambia neema yake yatosha  sasa uchaguzi uko juu yako Unapoichagua njia ya Mungu basi ni lazima uamue kwa dhati kupingana na sauti za shetani  ni lazima ukatae kujilaumu na kulaumu wengine ni lazima upingane na shetani kwa maneno ya ushindi anapokuambia wewe ni dhaifu sema mimi ni shujaa songa mbele kwa imani bila kuangalia nyuma  hii ndio njia pekee ya kumpinga shetani unapogundua kwamba ulifanya maamuzi mabaya.
  INAENDELEA.........
  Emmanuel Mwakyembe –MR. YOPACE
  +255716531353
  emamwakyembe@gmail.com