• Isikupite Hii

  December 7, 2017

  Ugonjwa wa goita dalili na tiba yake.


  UGONJWA WA GOITA DALILI NA TIBA YAKE
  Huu ni uvimbe usio wa kawaida katika kikoromeo(Thyroid Gland) ambao hutokea mbele ya shingo)

  Dalili za upungufu wa madini joto mwilini (Goita)

  i. Uvimbe mbele ya shingo
  ii. Mama wajawazito kuharibu mimba
  iii. Kudumaa mwili na akili
  iv. Mtoto kufia tumboni
  v. Kuzaliwa mtoto njiti (uzito pungufu au premature)
  vi. Kutetemeka na kuwa na wasiwasi.
  vii. Macho kutoka nje


  Sababu za kupata upungufu wa madini joto mwilini.

  i. Kupungua kwa IODINE katika chakula
  ii. Lishe duni


  Jinsi ya kuzuia upungufu wa madini joto mwilini
  i. Kutumia chumvi yenye Iodine (ayodini) hasa ile ya baharini
  ii. Kutumia vyakula vyenye Iodine(ayodini) kwa wingi kama vile dagaa, maziwa nk.
  iii. Kutoa elimu ya afya kwa jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora na
  iv. Kumpeleka mgonjwa hospitali iwapo ameshaanza dalili


  Matibabu ya upungufu wa madini joto mwilini

  i. Mgonjwa ataagiziwa dawa ya Iodine na daktari
  ii. Tumia dawa kama utakavyoagizwa na daktari
  iii. Operesheni itakayofanyika kama tezi imekuwa kubwa na athari zake zimeonekana