• Isikupite Hii

  HAWA NDIO WEZI 13 WAPUMBAVU ZAIDI DUNIANI

  7. Mwanamume aliyewatania polisi Facebook
  Mhalifu mtoro alijidhani alikuwa mjanja sana na akashawishika kuwacheza polisi wa Gwent, Uingereza waliokuwa wamepakia ujumbe kwenye Facebook wakiomba usaidizi kutoka kwa umma kumkamata Februari mwaka jana.
  Logan James, aliyekuwa na umri wa miaka 19 alikuwa akitafutwa kwa kukiuka masharti ya kuachiliwa kwake jela. Kijana huyo kutoka Caerphilly alikuwa awali amefungwa kwa kuwajerushi na kuwashambulia watu na pia kuwa na kisu. "Haha nishikeni iwapo mnaweza, hamtajua nikiponyoka,” aliwacheka. Baadaye aliambia shirika la habari: “Nimekuwa nikitembea karibu na nyumbani kwangu kwa hivyo hawajatia bidii kunikamata.” Image copyrightWales News Service Alikamatwa baadaye siku hiyo. Polisi walimshukuru kwa kuwasaidia kumkamata. 

  8. Mwizi aliyeshindwa kufungua mlango 
  Mwizi mwingine James Allan alinaswa kwenye kamera ya CCTV akitekeleza wizi katika duka moja Abingdon, Oxfordshire mwaka 2012. Ingawa hakutaka kuonekana uso wake, aliangukia mtambo wa kuhifadhi vinywaji na mwishowe akalazimika kuivua barakoa yake kutoka kichwani. Alijaribu kufungua mlango atoroke lakini akashindwa kwani badala ya kuuvuta mlango, alikuwa anausukuma. Mwanamke ambaye mwizi huyo alikuwa amemzuilia akitumia bunduki bandia ndiye aliyemsaidia kuufungua mlango huo. Isitoshe, Allan aliyekuwa na umri wa miaka 29 wakati huyo, alikuwa amejaribu kuiba kutoka kwenye duka hilo siku 10 awali. Alifungwa jela miaka mitatu kwa kosa la wizi, miaka miwili kwa kuwa na silaha au mwigo wa silaha. Vifungo hivyo alitakiwa avitumikie sambamba. 

  9. Mwanamume aliyetumia mfuko kujifunika 
  Mwizi mmoja Christopher Badman, kutoka Bridgend kusini mwa Wales, alitumia mfuko wa kubebea bidhaa kuficha kichwa chake alipokuwa akitekeleza wizi katika hoteli moja Porthcawl wakati wa mkutano wa kumkumbuka Elvis Presley. Alishawishika kutoa mfuko huo kichwani alipokuwa ameangalia kamera ya CCTV. Polisi walimtambua kwa urahisi na kumkamata. Badman alikiri kuvunja na kuingia kwenye hoteli hiyo na akatakiwa kulipa £900 kama na £100 juu. 

  10. Jambazi akwama dirishani 
  Mwizi mmoja nchini Uchina alihitaji kusaidiwa na watu baada yake kukwama kwenye dirisha nyembamba akijaribu kuingia kwenye nyumba moja ghorofa ya tano. Alishindwa na kubaki amening’inia. Iliwachukua waokoaji dakika 30 kumuokoa. Alikabidhiwa kwa maafisa wa polisi. 

  11. Mwizi wa benki aliyeacha anwani yake
  Mwizi wa benki aliyejaribu kujificha kwa kuvalia miwani ya giza n ahata kuvalia soksi juu ya viatu vyake, alisahau kwamba alikuwa ameacha anwani yake. Dean Smith, 27, alikuwa ameenda kwenye tawi la benki ya Barclays eneo la Treorchy, Wales kubadilisha anwani yake alipovutiwa na pesa zilizokuwa kwenye meza.
  SmithImage copyrightWales News Service Image caption Smith baadaye alikiri kwamba alikuwa "mjinga sana" Alirejea baadaye akiwa amevalia miwani hiyo ya giza na soksi na kumtaka keshia ampe pesa hizo. Keshia alikataa na akalazimika kutoroka mikono mitupu. Polisi walimpata kwa njia rahisi baada ya kufuatilia video ya kamera ya CCTV, wakamtambua na kisha kufahamu anwani yake. Alikiri kwamba alikuwa “mjinga sana”. Alifungwa miaka miwili unusu. 

  12. Mwizi wa gari azimwa na auto-lock 
  Mwizi wa gari katika mji wa Pretoria, Afrika Kusini, alizimwa baada ya mfumo wa kufunga gari wa auto-lock kulifunga gari baada yake kuingia ndani. Alikwama kwa saa moja unusu akiitisha usaidizi. Wapita njia walimcheka tu hadi mwenye gari aliporejea, akiwa ameandamana na polisi, kwa mujibu wa gazeti la The Star. "Unafanya nini ndani ya gari langu?” alimwuliza mwenye gari kabla ya kumfungulia, na polisi walioandamana naye wakamkamata mara moja. 

  13. Simu ilivyomponza mwizi

  Wezi wengi wamekamatwa kutokana na picha za kujipiga, yaani selfie, na Ashley Keast, bila shaka hatakuwa wa mwisho. Alitumia laini ya simu aliyokuwa ameiba kujipiga picha akiwa ndani ya nyumba ambayo alikuwa amevunja na kuingia 2014. KeastImage copyrightSouth Yorkshire Police Image caption Ashley Keast Mwanamume huyo kutoka Rotherham baadaye alipakia picha hiyo kwenye Whatsapp lakini bila kujua akamtumia mfanyakazi mwenzake mwenye nyumba aliyokuwa amevunja. Maafisa wa polisi walimpata kwake nyumbani akiwa na saa aina ya Rolex ya thamani ya £4,000 aliyokuwa ameimba. Keast, aliyekuwa na umri wa miaka 25 wakati huo, alifungwa jela miaka miwili na miezi minane baada ya kukiri kosa la kuvunja nyumba na kutekeleza wizi. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

  Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.