• Isikupite Hii

  May 1, 2014

  FAHAMU MENGI KUHUSU GAZUKO NA MZIKI WAKE

  Unaweza ukawa umewahi kumsikia au kumshuhudia  akifanya mambo jukwaani lakini ukawa haujajua mambo mengi kuhusu Amos Savin Gazuko,rapper wa injili ambaye amekuwa gumzo kutokana na pilika pilika nyingi ambazo anafanya,mara utasikia The night of Gazuko na vinginevyo ikiwemo blog kadhaa anazozimiliki.
   Wiki hii rappa Gazuko alijikuta akiwa na furaha zaidi baada ya kugundua wimbo wake wa Acha kulia umeweza kusikilizwa na watu zaidi ya buku na kupakuliwa na na watu wasipongua jiti tatu..
   Leo niliweza kupata wasaa na kupiga nae story mbili tatu kuhusiana na maisha pamoja na mziki wake na alijibu maswali kadhaa kama ifuatavyo...

  Tim heaven(HT);Kwanza kabisa hongera kwa nyimbo yako kuchezwa na kupakuliwa kwa wingi,nini siri ya mafanikio yako?
  Gazuko:aah,ni kujitambua,kujituma pamoja na support za wadau

  TH:Gazuko umekuwa moja kati ya rappers gumzo sana kwa sasa,tungependa kujua umetokea kwenye familia ya aina gani na ina mchango gani kwa kile unachokifanya?
  Gazuko:Nimetokea kwenye familia ya kilokole..hapo awali ilikua ngumu saana familia yangu kunielewa na hawakuwa na imani na kile ninachofanya,mpaka ikafika kipindi wazazi wakathubutu kuniambia kuwa sitofika popote hivyo niachane na muziki lakini pamoja na hayo nilisimama katika harakati hizi za gospel hiphop,ninamshukuru MUNGU imefika hatua wazazi wangu wameelewa nini nafanya kutokana na hatua niliyopiga..

  TH:Ilikuaje mpaka ukaanza kufanya muziki?
  Gazuko:Nilikuwa nina kila sababu ya kufanya muziki kwa sababu ni kipaji ambacho ninacho tangu kuzaliwa.

  TH:Nani alikwambia au ulijuaje kuwa una kipaji cha muziki?
  Gazuko:Awali nilikuwa nina copy nyimbo za bongo flavour,lakini mtaani kwetu kulikuwa na msanii mmoja anaitwa Abdul Mkami maarufu kama KALI P, aliyekuwa akitamba na wimbo wa Imekaa vibaya,baada ya Kali P kutoka nikaona kumbe na mimi Gazuko ninaweza kutoka nikafanya muziki mimi kama mimi,ndipo nikaanza kufanya muziki wa bongo flavour nikiwa na kundi la Best Boyz  na wenzangu kama Side ambaye kwa sasa anafanya Sanaa za maigizo na Shizzle ambaye alikuwa dancer wa A.Y ambaye kwa sasa nahisi yupo T.H.T.

  TH:Sasa ilikuaje ukaanza kufanya muziki wa injili?
  Gazuko:kwanza tambua kuwa nimetokea kwenye familia ya kilokole,lakini mwaka 2001 nilianza utukutu na kutoroka nyumbani hadi nikaamua kuishi maisha kama mtoto wa mtaani nikilala kwenye nyumba zisizoisha,lakini  mwaka 2008  neema ya Bwana ilinitembelea na kujikuta nimerudi kundini ila yote kwa yote niliokolewa kupitia muziki wa gospel hiphop,nami nikaona kuwa naweza kufanya gospel hiphop ili kuhakikisha kuwa Mungu anabadilisha maisha ya vijana kupitia Hiphop,Hiyo ndiyo sababu ya mimi kufanya muziki wa injili.


  TH:Ilikuaje mpaka ukaokolewa kupitia muziki wa Hiphop?
  Gazuko:Ilikua mwaka 2007 mwishoni kulikuwa na mkutano wa muhubiri Egoni Faki kutoka huduma ya NewLife Outreach,miongoni mwa waimbaji waliomba ni Obby family wakiongozwa na Pona,walichana wimbo ulioitwa Watalia meeeh meeh hawatasamehewa ,kiukweli tangu pale nilipousikia ule wimbo ulifamyika kuwa mbegu ndani yangu,mwaka 2008 mwanzoni nikaamua kurudi kundini

  TH:Wewe kama Gazuko una malengo gani katika muziki wako..?
  Gazuko:Malengo ni mengi lakini siwezi nikayaweka hadharani maaana kuna vitu vya sirini na vya kuweka hadharani,kikubwa ni kwamba wadau wangu wakae mkao wa kula,maana Gazuko wa jana sio yule wa leo na wa kesho pia

  TH;Kama muimbaji unaonaje maendeleo ya muziki wa injili hasa Gospel hiphop?
  Gazuko:Gospel Hiphop kwa sasa ipo katika level nzuri na imepata kibali cha kutosha maana mpaka inafika waimbajiengi wanatamani kuhama kutoka kwenye muziki wa kawaida kuja kufanya hiphop na wengine wameamua ku mix na hiphop,hii inaonyesha ni jinsi gani hizi harakati zipo katika eneo zuri..

  TH:Unadhani ni kitu gani kimefanya muziki wa gospel hiphop kupata kibali kiasi hiki?
  Gazuko:Ni Mungu mwenyewe lakini pia na mfumo mzima wa muziki ulivyo,sasa hivi watu wanahitaji mabadiliko na ndio maana leo hii ikitokea tamasha ukampandisha  Rungu la Yesu aka perform halafu ukampandisha mwimbaji wa kawaida,kiukweli inahitajika huyo mwimbaji awe amejipanga kwelikweli,pia harakati hizi zimepata kibali kutokana na jumbe zilizopo katika nyimbo hizi

  TH:Je wewe kama Gazuko unaufanyia nini muziki wa injili kuhakikisha unazidi kupaa?
  Gazuko:inapokuja swala kama hilo ni mipango binafsi ambayo siwezi kuiweka hadharani..

  TH:Unachukuliaje ukuaji,ubora na uhai wa mziki wako?
  Gazuko:Hilo swali unapaswa uwaulize mashabiki wangu

  TH:Muziki unaofanya umekupa faida gani?
  Gazuko:Ninamshukuru Mungu kupitia mziki umenifanya nijuane na watu wengi pia nmepata nafasi ya kuwa karibu na wasanii ambao zamani nilikua nawasikia redioni na kuwataza kwenye TV lakini leo nina uwezo wa kuonana nao popote pale ninapotaka,pia nnapohitaji kitu nna uhakika wa kukipata hiyo yote ni matunda ya muziki..

  TH:NI waimbaji gani wanaokuvutia ndani na nje ya tanzania(watano kila sehemu)
  Gazuko:kwa Tz waimbaji nnaowakubali saana ni
   1.happy kamili
  2.Bashando
  3.Rungu la Yesu
  4.Leah Amos
  5.Stevene Mwikwabe
  Nje ya Tz ni
  1.Ephraimu Sekeleti-Zambia
  2.Dady Owen-Kenya
  3.Kirk  franklyn-U.S.A
  4.Isack Molgan-Uganda
  5.Lundi-South Afrika

  TH:kwa kumalizia una waambia nini mashabiki wako?
  Gazuko:Mashabiki wangu wajipange kwa ujio wa Gazuko kwa maana nimewaandalia tamasha kubwa la Nanena Concert nitazidi kuwajuza kadri mambo yatakavyokuwa..