• Isikupite Hii

  May 23, 2014

  MJUE BASHANDO KINAGAUBAGA... UZINDUZI WAKE TAREHE 25 MAY 2014

                    Martin Shaboka Marwa A.K.A Apostle Bashando,rapper aliyebebea ma-credit mengi katika tasnia ya muziki wa injili hususani kwenye mahadhi ya Hiphop kutokana na uandishi wake wenye ubora kuwahi kutokea katika tasnia hiyo.
                  Rapper Bashando alianza kujipatia umaarufu miaka ya nyuma baada ya kazi zake kama Punga mikono na zinginezo kuweza kuwepo katiaka collection ya Amen volume 1&2.
                Baada ya kimya kirefu sana,sasa Bashando ameibuka na project mpya ambayo ni uzinduzi wa album yake ya kwanza kabisa kuwahi kutokea katika maisha yake ambayo inakwendwa kwa jina la NAONGOZWA NA ROHO atakayo izindua jumapili ya tarehe 25/5/2013 katiaka ukumbi wa MSB hall pale kituo cha Mbuyuni kabla ya Tegeta,Martin Bashando aliwakaribisha wadau wote wa mziki na kiingilio kitakuwa ni bure ,pale tulipokutana maonezi yetu yalikuwa kama ifuatavyo;

  TIMHEAVEN: Watu wengi wameanza kukufahamu kwa wingi katika collection za ameni volume one n.k,lakini tungependa kufahamu ni lini hasa bashando umeanza kufanya mziki huu na ilikuaje ukaanza kuimba?"


  Bashando:  Kwanza kabisa nmetokea familia ambayo ni wapenzi wa muziki na pia ina wanamuziki,nilipokuwa mdogo mama yangu alikua akituma kununua matoleo ya kanda ya miziki ya enzi hizo jambo ambalo lilinifanya niwe mpenzi wa muziki.Nakumbuka kipindi niko darasa la nne nilikuwa nina uwezo wa kushika na kuimba nyimbo za Dr.Remmy Ongala.  

        Mwaka 1996 ndipo nilianza kusikiliza nyimbo za sugu ana kuvutiwa nazo na mwaka 1999 ndipo nilipoanza kujfunza kuandika mashairi japo sikuwa serious na kufanya muziki,ila baada ya Nigga J kutoka na kibao cha chemsha bongo mwaka 2000 pale ndipo niliposhawishika  kujikita kwenye bongo fleva hadi mwaka 2001 professa Ludigo aliponiwashauri nianze kuimba gospel hiphop ambapo ndipo safari yangu ya mziki ilipoanzia  TIMHEAVEN: umesema umetokea kwenye familia ya wanamziki,una ndugu wengine ambao ni wasanii?

   Bashando: Bishop Nickodemus ni mwanamziki,kuna mr.teacher,Bob dunda hao wote ni ndugu zangu,isitoshe hata baba mara nyingi alikuwa akitufundisha kuhusu mziki.

  TIMHEAVEN: professa ludi ndiye aliyekushawishi kufanya mziki wa injili,ilikuaje akushawishi kuachana na bongo fleva uliyokuwa ukifanya uanze kufanya mziki wa injili?sababu nyuma yake?

   Bashando: Wakati huo nilikua naimba Bongo fleva huku nimeokoka ndio prof ludi akaniambia  ni bora kuhubiri kupitia hiphop kuliko kuendelea kuimba bongo fleva huku nmeokoka

  TIMHEAVEN: Bashando kwa miaka unayoongolea hapa,inaonyesha kipindi hicho professa Ludigo alikua ni producer anayehusudiwa  sana,ilikuaje ulipata chance ya kuwa karibu na jamaa ikiwa ulikuwa bado kinda kwenye game.

  Bashando: Prof. Ludi ni rafiki yangu ambaye nilifahmiana naye kupitia mdogo wake,kagisa ambaye tulikuwa tunasari wote pale chuo cha manabii.

  TIMHEAVEN: Kwa kipindi chote ambacho ulikuwa unafanya bongo fleva je ulifanikiwa kurekodi?je ni wasanii ganii wa bongo fleva ambao ulikuwa  unawahusudu saana ufanye nao kazi?

  Bashando: Sikuwahi kurekodi bongo fleva maana nilifanya maaamuzi ya kugeuka mapema saana.wasanii niliotamani kufanya nao kazi walikua ni Prof.jay,fid q na afande sele.

  TIMHEAVEN: Kuna wakati ulikuwa uko katika harakati na kikundi cha dotcom generation,je mmefikia pamoja na album yenu ya Awamu nyingine

  Bashando:  Kundi la dotcom generation lipo lakin bishop nickodemus shaboka mmoja kati ya waundaji wa kundi hilo,amekuwa busy saaana na kuhubiri jambo ambalo limefanya muda mwingi niwe peke yangu,na album ya Awamu nyingine bado ipo..

  TIMHEAVEN: Baada ya ameni volume two,kuna wakati ulikuwa ziii,vipi kuhusu hilo..ulikua wapi na baada unafanya nn?

  Bashando: Maisha  yaliniendea vibaya sana kiasi  kiasi kwamba nilakaribia kudata hivyo kuyaweka mambo sawa ilinibidi nipotee kidogo na kuanza kutafuta hela kwanza..ndio maaana nikawa kimya

  TIMHEAVEN: unadhani ni kikwazo gani kinachosababisha mpaka ushindwe kufaidi matunda ya mziki wako?

  Bashando: Mziki wangu nnaufurahia na nimeshafaidi vitu vingi tu kupitia huo lakini kikwazo kama kama kinaishia hv sitopenda kukiongelea