• Isikupite Hii

    June 21, 2014

    RAPPER GAZUKO ANAACHA KULIA MWISHO WA MWEZI HUU

    Baada ya kuachia  kideo kikali cha Acha kulia,kwenye mtandao wa video wa youtube,Rapper anayetesa maskioni mwa wengi kwa sasa Amos Savin Gazuko,ameandaa tamasha rasmi kwa ajili ya kukizindua rasmi kideo hicho chenye kiwango cha juu ambacho kilifanyika chini ya kampuni ua Kingdom Media ya Marekani ikiwa Bwana Alex Joseck ndiye muongozaji mkuu katika video hio..

    Kwa mujibu wa taarifa toka mitandao mbalimbali ikiwemo facebook account ya Gazuko mwenyewe,tamasha hilo litafanyika siku ya jumapili tarehe 29/06/2014 katika ukumbi wa  Heroes Hotel,muda ni kuanzia saa 8 mchana na kuendelea ambapo atasindikizwa na waimbaji wengi wanaoitikisa kwenye mziki wa injili kwa sasa kama Rungu la Yesu,MArtin Bashando,Magele ana wengine wengi..Bwana Gazuko anapenda kuwakaribisha katika tamasha hilo ambalo halina kiingilio.