• Isikupite Hii

  June 18, 2014

  RUNGU LA YESU AMPA SHAVU MUME MTARAJIWA WA ROSE MUSHI

                                     Rungu la Yesu katika pozi na mtangazaji wa Wapo radio,Silas Mbise..

  Baada ya kuianza safari toka mbinga mpaka Dar kisa Injili,sasa Rungu la Yesu anaendeleza safari kwa kuachia jiwe jingine hivi karibuni.
        Kupitia facebook account yake rapper Rungu la Yesu,anayetamba na ngoma kadhaa kwa radio na mitandao kama vile Bwana Yesu asifiwe na Naanza safari,amebainisha kuwa yuko mbioni kuachia ngoma nyingine mpya ambayo itaambatana na ujio wa project kubwa saana ya Yesu Okoa mitaa.

  Rungu ambaye pia ameachia video ambayo inamuonyesha akichana nyimbo hiyo akapela,amebainisha kuwa amemshirikisha jamaa mbaya saana kwenye michano na R&B,A.K.A Bishop,A.K.A mume mtarajiwa wa mwanadada  Rose Mushi,si Mwingine bali Nickodemus Shaboka,ambaye amesimama kwa chorus mwanzo mwisho kuhakikisha kuwa hakuna kwa kupoteza.
  Jamaa hajataja tarehe rasmi ila amehaidi itakuwa mwanzoni mwa mwezi na jina la wimbo unaitwa ilikua zamani..
            Bwana Nickodemus Shaboka na mchumba wake Rose Mushi,anayetarajiwa kufunga nae ndoa karibuni