• Isikupite Hii

  January 4, 2015

  KWA NINI MUNGU HAKUMWARIBU SHETANI BAADA YA SHETANI KUASI??

      

            Hili Ni Swali Ambalo Liko Katika Vichwa Vya Watu Wengi Sana, Kwamba Ni Kwa nini MUNGU Hakumfutilia Mbali Shetani Baada Ya Shetani Kuhasi. Wote Tunajua Kwamba Kuna Siku Shetani Atatupwa Katika Ziwa La Moto Na Kiberiti Na Shetani Atateswa Huko Mchana Na Usiku. (Ufunuo 20:10). Mimi Na Wewe Wote Hatuna Uhakika Ni Kwa Nini Hasa Lakini Tunajua Jinsi Mungu Anavyotenda Kazi.


            Kwanza Kabisa MUNGU Wetu Ni MUNGU Mwenye Mipango Na Mipango Yake Ni Thabiti. Anajua Ni Wakati Gani Afanye Nini Na Nini Asifanye. Hukumu Zake Ni Za Haki Kwa Sababu Yeye Ni MUNGU Wa Haki. Lakini Pia Wote Tunajua Kwamba MUNGU Yuko Na Mamlaka Juu Ya Viumbe Vyote Mbinguni, Dunia, Na Hata Kuzimu. Na Tunajua Kwamba MUNGU Alishapanga Kila Kitu  Kuanzia Mwanzo Mpaka Mwisho. Hakuna  Mtu Anaeweza Kufuta Mipango Ya Mungu, Kila Kitu Kinaenda Kama Alivyo Panga Yeye Mwenyewe. (Isaya 14:24) "BWANA Mwenye Nguvu Ameapa, Hakika, Kama Vile Nilivyopanga Ndivyo Itakavyokuwa, Nami Kama Nilivyokusudia Ndivyo Itakavyosimama". 

          Mwisho, Siku Zote MUNGU Hutuwazia Yaliyo Mema. Yeremia 29:11. Na Sizana Kama Ni Jambo la Hekima Sana Kuhoji Kwa Kukosoa Ama Kutia Shaka Juu Ya Hukumu Za MUNGU, Tabia Zake Na Hasiri Yake Kwa Ujumla. Yeye Ana Haki Ya Kufanya Kile Anachotaka. Mzaburi Anasema (Zaburi 18:30)"Huyu MUNGU Matendo Yake Hayana Dosari, Ahadi Zake Niza Kuaminika". Mpango Wowote Utokao Kwa MUNGU Ndio Mpango Unaofaha. Isaya 55:8-9 "Kwa Kuwa Mawazo Yangu Sio Mawazo Yenu, Wala Njia Zenu Si Njia Zangu" Asema BWANA. 9. Kama Vile Mbingu Zilivyo Juu Kuliko Dunia, ndivyo Njia Zangu Zilivyo Juu Kuliko Njia Zenu Na Mawazo Yangu Kuliko Mawazo Yenu." Jukumu Letu Ni Kumtii Mungu, Kumwamini Yeye, Na Kuyakubali Mapenzi Yake Juu Ya Maisha Yetu Tuwe Tunayaelewa Ama Atuyaelewi. Yeye Ndiye Ajuae Ni Wakati Gani Wa Kummalaza Shetani Na Majeshi Yake.    Pia Na Wengine Wanasema Kwamba MUNGU Akumwondoa Shetani Baada Ya Shetani Kuasi, Ili Ajue Ni watu Gani Wanaompenda  Yeye MUNGU Kweli Kweli.