• Isikupite Hii

  February 25, 2015

  MUSIC: SHUKURANI ZANGU - NEEMA LYIMO WA MNG'ONG'O.  Naitwa Neema Lyimo wa Mng'ong'o. Hapo Mwanzo nilijulikana kama Neema Lyimo lakini sasa nimeolewa na Mr P. Mng'ong'o ndiyo maana jina limebadilika kidogo na kuitwa Neema Lyimo wa Mng'ong'o.

  Mara ya mwisho nilifahamika kwa wimbo wa "Tuvuke Ng'ambo", Na baada ya apo nikawa kimya kwa muda mrefu sana kwa sababu niliingia kwenye ndoa, nikalazimika kuacha majukumu ya uimbaji na kuwa na familia yangu kwanza. Katika kipindi hicho, nikalea ujauzito kwa miezi tisa na kisha tukajaaliwa mtoto mzuri sana wa kiume anaitwa Ethan Paul Mng'ong'o. Kwa kipindi kirefu kisichopungua miezi sita nilikaa na mtoto tu na baada ha hapo ndipo nilipopata kibali na kurejea kwenye huduma.

  Ninamshukuru Mungu kwa kunipa mume ambaye anaipenda sana huduma yangu na kwa kweli anani-support katika kila hatua. Yeye ameniwezesha kufanya album nyingine ambayo itatoka hivi karibuni, na sasa nimeanza mipango ya kurecord video. Baada ya kukamilisha hayo yote ndo nitarelease hiyo album yangu mpya. Sasa hivi media zimeanza kupiga nyimbo zangu hasahasa unaopigwa sana ni wimbo unaoitwa "SHUKURANI ZANGU"

  Mungu akubariki sana. Ninachokuomba mtu wa Mungu ni kitu kimoja, Uniombee ili Mungu aendele kunisaidia niwe na Uadilifu na tabia njema (Integrity and good Character) ili kabla sijahudumu, nimpendeze Mungu, familia yangu na wanadamu n Mungu anitumie katika kuujenga ufalme wake.

  Mwisho kama unahuduma ya Mungu popote pale, Mkutano wa Injili, Semina, Ibada nk, tushirikiane wala usiogope kunialika ili tujenge pamoja ufalme wa Kristo. Mambo ya fedha na gharama usiyafikilie kwanza, Mungu alinipa kazi na huduma hii bure kabisa, jambo la kwanza tumtumikie Mungu kwa urahisi ili kuujenga ufalme wa Mungu mengine Mungu atatupatia kwa wingi na kwa jinsi anayoijua yeye.

  Click Hapa Kutembelea Na Kulike Ukurasa Wa Facebook Wa Neema Lyimo wa Mng'ong'o.

  Mawasiliano Zaidi:-
  Namba +255 753 777 057
  E-mail: neemamngongo01@gmail.com
  Facebook:  Naitwa Neema Lyimo wa Mng'ong'o.