March 31, 2015

HALI (AFYA) YA ASKOFU GWAJIMA YAZIDI KUIMARIKA


Hali ya mchungaji kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Askofu Josephat Gwajima aliyelazwa katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam inazidi kuimarika. Taarifa kutoka kwa watu wake wa karibu inasema mchungaji Gwajima amehamishwa kutoka chumba cha wagonjwa mahututi kwenda chumba cha kawaida ambapo mwenyekiti wa chama cha siasa cha wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba ni mmoja kati ya watu waliofika hopsitali siku ya leo kumjulia hali mchungaji huyo.


Hima kwa Wakristo na wenye mapenzi mema kuendelea kumuombea mchungaji huyo ili hali yake izidi kuimarika na kuendelea na shughuli zake za kuhubiri injili na kuleta mabadiliko katika jamii yetu ya Tanzania na dunia kwa ujumla. Askofu Gwajima alikimbizwa hospitalini hapo toka siku ya ijumaa usiku baada ya kudaiwa kuzimia alipokuwa akihojiwa na kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova ofisini kwake.

Source: GospelKitaa.