• Isikupite Hii

  March 9, 2015

  MAAJABU: MCHUNGAJI AWATAKA WAUMINI KUMSHUKURU MUNGU UWEPO WA BANGI

  Katika hali isiyotarajiwa na wakristo waliowengi na kuonyesha kuwa ule mwisho umekaribia, ni kwamba mchungaji Chris Schuller wa kanisa la Episcopal la Mtakatifu Thomas huko St Petersburg Florida nchini Marekani kupitia video yake aliyoweka kwenye mtandao wa Youtube amewataka watu kuacha kujaji na kuwarushia maneno wavuta bangi na badala yake wamshukuru Mungu uwepo wa Marijuana ama bangi.

  Video hiyo ambayo iliwekwa na mchungaji huyo mwezi December mwaka jana imechukua sura mpya siku za karibuni baada ya kuonwa na askofu mkuu wa kanisa hilo Dayosisi ya kusini magharibi mwa Florida Dabney Smith ambaye imeelezwa kumchanganya na huenda mchungaji huyo akachukuliwa hatua hivi karibuni kwa kitendo chake cha kutoa neno kwenye jamii lenye kuunga mkono utumiaji wa madawa.

  Kwa mujibu wa msemaji wa dayosisi hiyo Garland Pollard katika mahojiano yake na The Tampa Bay Times amesema katika zama hizi za mitandao ya kijamii kuna kofia mbili ambazo watu wanazivaa na kwamba amesema kuna haja ya kufikiria namna ya kujitambulisha wajihi wetu, kwakuwa cheo cha uchungaji alichonacho ni cha juu alisema Pollard. Katika video hiyo ambayo mchungaji Chris Schuller ameipa jina la 'Thank God for Marijuana' ameeleza kwamba utumiaji wa dawa hizo ni sawa na unywaji wa bia ama mvinyo katika kujipumzisha.

  "Hakuna mtu anayeonekana kuwa na tatizo utumiaji wa bia ama mvinyo. lakini mamilioni ya watu wameonyesha kuwa na matatizo utumiaji wa bangi, badala yake tungemshukuru Mungu uwepo wa bangi kwakuwa ni njia moja wapo aliyotupa Mungu katika kujipumzisha na kupata nguvu…… kumsifu Mungu kuna leta hisia nzuri zaidi kuliko kujaji watumiaji" amesema mchungaji Schuller katika video hiyo ambayo urefu wake ni dakika 2 na sekunde 15.

  Aidha wakati askofu Smith anapanga kumuadhibu mchungaji wake kwa kitendo hicho mchungaji Schuller ametangaza kuachana na kanisa hilo katika tamko lake aliloweka kupitia ukurasa wake wa Facebook akisema kama alivyoitwa na Mungu kufanya huduma chini ya dhehebu hilo hata sasa hivi anahisi Mungu amemwita kufanya kazi nje ya ambako atakuwa na uhuru zaidi na huduma yake.
  Mtandao wa Kikristo wa ChristianPost umeandika habari hii 


  Chini ni maelezo ambayo yanapatikana katika ukurasa wake wa Facebook wa mchungaji huyo, huku picha yake pia ikimuonyesha yupo bize na uvutaji.