April 1, 2015

NYOTA WA MUZIKI WA INJILI AMJIA JUU MCHUNGAJI ALIYEWATAKA WAUMINI KUMNUNULIA NDEGE YA KIFAHARI.


Aina ya ndege ambayo mchungaji huyo amewataka waumini wake wamnunulie.

Nyota wa muziki wa injili duniani Kirk Franklin wa nchini Marekani imembidi kuingilia kati kutoa maoni yake juu ya mchungaji Creflo Dollar ambaye amewataka waumini wake wamnunulie ndege ya kifahari aina ya Gulfstream G650 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 65 sawa na shilingi bilioni 119 kwa ajili ya huduma yake.

"Mchungaji kuwataka waumini wamnunulie ndege binafsi wakati wahubiri wanaogelea kwenye maumivu ni ukosefu wa utu, nikitanguliza tamaa yangu ili ionekane kama hitaji, huo ni ukosefu wa utu" alisema Franklin kupitia chapisho la blog ya Patheos yenye kichwa cha habari "Gharama kubwa ya utu".

Kitendo cha mchungaji huyo  kiliamsha hisia zaidi kwa wananchi ambao walianza kujitokeza wakipinga mpango wa mchungaji Dollar  ambaye ni mwanzilishi wa huduma ya World Changers Church International ya kuchangisha dolla milioni 65 za kimarekani kutoka kwa watu laki mbili ili kununua ndege hiyo.

Kirk kushoto pamoja na mchungaji Creflo Dollar
Mambo yalizidi kwenda vibaya zaidi siku ya jumatatu baada ya watu walioanzisha kampeni ya kupinga mpango wa mchungaji huyo kama ilivyoripotiwa na mtandao wa The Christian Post kuzidi kuongezeka wakilazimisha huduma ya mchungaji huyo kusimamisha zoezi lao la uchangishaji pesa za kununulia ndege hiyo. "Kwasasa hakuna kampeni hiyo tena" alisikika akisema Juda Engelmayer wa 5W inayojihusisha na mambo ya mahusiano na jamii (Public Relations), kitengo ambacho kilikuwa kinamwakilisha mchungaji huyo katika zoezi la kuchangisha pesa hizo kama alivyohojiwa na Christian Post siku ya Jumatatu. 

Ambapo mpango wa kusimamisha zoezi la uchangishaji fedha ulifanikiwa ikiwa pamoja na tovuti iliyokuwa imefunguliwa rasmi kwa ajili ya zoezi hilo kuzimwa hewani. Hata hivyo licha ya kusimamisha zoezi hilo Engelmayer amesema mchungaji Dollar kwasasa amekazia kwenye kufundisha kuhusu Yesu na Biblia na kuondokana na kusimangwa ila ikitokea wakapata bei nzuri na nia bado basi watanunua ndege hiyo.

Christian Post imeripoti