Featured Posts

April 17, 2015

NEWS: KANYE WEST AZINDUA BIBLIA YAKE NA KUJIITA MUNGU.


Hujulikana sana kwa maringo yake, lakini Kanye West amefanya makosa kubwa sana kukufuru na kujitambulisha kama mungu katika Kitabu Chake Hicho Anachokiita biblia.


Kitabu hicho anachokiita "The book of yeezus A Bible for the modern day" yani "Kitabu cha yeezus biblia kwa kizazi kipya". Amini usiamini kila neno la Mungu katika kitabu hicho limeondolewa na badala yake msanii huyo wa muziki wa kufoka foka ameweka jina lake.
Kulingana na gazeti la The Independence nchini Uingereza, kitabu hicho kinasema kuwa katika kizazi hiki , Kanye West ndio mkubwa na vilevile kiongozi wa kidini
Kitabu hicho kinaongezea kwamba ''katika utangulizi wetu tunamsherehekea Kanye West na vile alivyotufanyia katika maisha yetu''


Ijapokuwa Kanye hajatoa tamko lolote kuhusu wadhfa huo aliojipatia, amekuwa akijifananisha na Mungu hapo mbeleni.
''Mungu alinichagua mie, alinitengezea njia.Mimi ni chombo cha mungu'', alisema mwaka 2009.
''Lakini kinachoniudhi maishani mwangu ni kwamba sitawahi kujiona nikicheza muziki moja kwa moja''.,aliongezea.
Wasanii wengine waliofananishwa na Yeezy ni Marilyn Monroe na Michael Jackson.

Mtu Wa MUNGU Unanini Cha Kusema Juu Ya Hili Swala La Uyu Jamaa Kujiita mungu Na Kuzindua Biblia Yake?

Comment Hapa Chini.......