April 17, 2015

NEWS: MAMIA YA WAUMINI WA KANISA LA GWAJIMA WAFURIKA NYUMBANI KWAKE BAADA YA TAARIFA ZA POLISI KUMZINGIRA.


Mamia ya waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima nchini lililochini ya Askofu Josephat Gwajima walikusanyika nyumbani kwa kiongozi wao huyo maeneo ya Salasala jijini Dar es salaam, mda mfupi uliopita baada ya kuwepo taarifa za jeshi la polisi likiwa na silaha za moto pamoja na magari wakiwa wameizingira nyumba hiyo huku taarifa hasa za kuhusu uvamizi huo zikiwa hazijajulikana bado.

Mda mchache uliopita mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo ametoa taarifa kupitia ukurasa wa Facebook wa kanisa hilo kuwajulisha waumini kwamba baada ya jeshi hilo kufika nyumbani kwa mchungaji huyo toka majira ya saa kumi za alfajiri hawakufanikiwa kuingia ndani kwakuwa uzio wa nyumba ya mchungaji huyo imewekewa umeme hivyo baada ya kuwepo takribani masaa kadhaa taarifa hiyo inadai askari hao wameondoka eneo la tukio mda mfupi uliopita na kumpa mwanya mchungaji huyo akiwa na wasaidizi wake kuondoka kwa maana ya sasahivi kuelekea polisi ili kuwauliza uwepo wao nyumbani kwake siku ya leo.

Source: Gospel Kitaa.