• Isikupite Hii

  April 4, 2015

  Kshs. 20 MILLION KUTOLEWA KWA ATAKAE MKAMATA GAIDI ALIEUSIKA KATIKA MAUWAJI YA WANACHUO 147 KENYA.

  Tayari wizara ya mambo ya ndani imetangaza dau la shilingi milioni 20 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kaw Mohamed Mohamud almaarufu kama Dulyadin, ama kwa jina lingine Gamadhere, kwa kuhusika na shambulizi hilo.


  Ilivyotokea
  Alfajiri ya Alhamisi, mida ya saa kumi na moja, njozi za watu zikiendelea usinginzini, huku wengine wakiwa kwenye maombi yao ya asubuhi, ndipo ghafla watu wanaoripotiwa kuwa wanne waliingia na kuanza kushambulia mabwenini huku wakihoji nani muislamu, na nani siye - ili kulenga shabaha zao vema. Limekuwa shambulizi la kigaidi kutoka kikundi cha Al-Shabaab (kama walivyodai wenyewe).

  Miili ya wasomi hawa ambao ni tegemeo kwa taifa la Kenya na dunia nzima kwa ujumla ilikuwa imetapakaa, wengine wakiwa na matundu ya risasi visogoni, ikionesha namna ambavyo walikuwa wanajaribu kujihami aidha kwa kulala chini ama kwa kukimbia popote pale katika juhudi za kujinusuru.


  "Tulichambua watu na kuwaachia Waislamu. Kuna miili ya Wakristo wengi waliokufa humo ndani. Pia tunawashikilia mateka wengi wa Kikristo. Mapigano yanaendelea humo ndani." Ananukuliwa Sheikh Abdiasis Abu Musab wa Al Shabab
  Japhet Malwa yeye kwa upande wake siku ilianza hivi. "Tulikuwa tumelala pale tuliposikia mlipuko wa bomu, na kisha risasi zikaanza kurindima. Kila mmoja wetu alikimbia kujaribu kujinusuru." Anaieleza Agence France-Press (AFP)

  Kuna ambao hawakuweza kukimbia mara moja na hivyo kukutwa na magaidi ambao waliwaua. Nina bahati kuwa hai kwa maana niliruka fensi. 

  Kwa upande wake Collin Wetangula anasema yeye alikuwa anajiandaa kwenda kuoga na ndipo ghafla akasikia milio ya risasi kutoka Bweni la Tana. Iliwabidi wajifungie pamoja na wenzake 4 kwenye chumba chao. Kwenye korido walisikia sauti za watu wakikimbia kimya kimya kuhofia kwamba iwapo sauti zitatoka basi wangejulikana walipo.

  Source: Gospel Kitaa.